Uhuru Kenyatta: Vifaa vya uchaguzi vilikuwa vichache

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amelaumu idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupiga kura kwa ghasia zilizotokea katika uteuzi wa chama hicho siku ya Ijumaa ambazo zilisababisha kufutiliwa mbali kwa shughuli yote.
Katika maeneo mengi nchini humo kulikuwa na uchelewashaji wa vifaa vya kupiga kura huku ghasia pia zikiripotiwa katika huku wagombea wakilaumiana kwa wizi wa kura.
Rais Kenyatta amekiri kwa maripota kulikuwa hakuna vifaa vya kutosha vya uchaguzi huo.

Uchaguzi huo ni maandalizi ya uchaguzi mkuu mnamo mwezi Agosti ambao utafanyika takriban miaka kumi kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi uliowaacha baada ya uchaguzi uliokumbwa na ghasia na kusababisha vifo vya takriban watu 1000 huku wengine nusu miliioni wakiwachwa bila makao.








