Tiger Woods afanyiwa upasuaji mwingine

Mcheza golf duniani Tiger Woods amefanyiwa tena upasuaji mgongoni ikiwa ni harakati za madaktari kutaka kumuondolea maumivu ya mgongo.

Kwa upasuaji huo sasa Woods anatarajiwa kuwa nje ya mchezo kwa takribani miezi sita. Huu ni upasuaji wa tatu katika eneo la mgongo wake ndani ya miezi 19.