Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maelfu waandamana Venezuela dhidi ya serikali
Maelfu ya raia wa Venezuela wameandamana katika mji mkuu wa Caracas na katika miji mingine zaidi ya 20. Waandamanaji wanataka kufanyike uchaguzi wa Urais na kuachiliwa huru kwa wanasiasa wa upinzani.
Wafuasi wa Rais Nicolas Maduro pia wamekua wakiandamana katika mji mkuu wa Caracas, kama ishara ya kumuunga mkono kiongozi huyo.
Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, Venezuela imeendelea kukumbwa na mfumuko mkubwa wa bei, visa vingi vya uhalifu na uhaba wa bidhaa muhimu.
Upinzani umelaumu serikali yenye kufuata mfumo wa ujamaa kwa matatizo ya sasa ya kiuchumi.
Msukosuko wa sasa wa kisiasa ulichochewa na hatua ya Mahakama ya Juu kutwaa mamlaka ya bunge ambalo linathibitiwa na upinzani.
Hata hivyo Mahakama ya Juu ilibatilisha uwamuzi wake baada ya kuzuka maandamano.
Kwa sasa Venezuela inashuhudia maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea kwa miaka mitatu