Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kamanda wa kikosi cha ulinzi wa rais I. Coast afungwa miaka 18 jela
Aliyekua kamanda wa kikosi cha ulinzi wa Rais{ Republican Guards}, nchini Ivory Coast amehukumiwa miaka 18 gerezani kutokana na mauaji ya mwaka 2011 mjini Abdijan.
Brunot Dogbo Ble na wengine tisa walipatikana na hatia ya utekaji nyara na mauaji ya wanaume wanne wakiwemo raia wawili wa Ufaransa katika hoteli moja.
Utekaji nyara huo ulifanyika wiki za mwisho za vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilizuka baada ya Laurent Gbagbo kung'angania madaraka licha ya kushindwa katika uchaguzi wa Urais mwaka wa 2010.
Aliyekua mkuu wa Polisi wakati huo Osee Longuey alihukumiwa miaka 20 jela.
Wanajeshi wengine wanne wa zamani walipata hukumu ya chini.
Kuna wengine ambao walipatikana bila makosa.
Taarifa zinasema mkuu huyo wa kikosi cha Ulinzi wa Rais aliwateka waathiriwa wake na kuwapeleka katika ikulu ya Rais ambapo waliteswa na kuuawa.