Mabaharia waiokoa meli iliyotekwa pwani mwa Yemen

Mabaharia kutoka India, Pakistan na Uchina wamewaokoa wafanyakazi katika meli iliyokuwa imetekwa nyara katika ghuba la Aden.

Meli hiyo iliyokuwa imetekwa na maharamia inapeperusha bendera ya Tuvalu na ilikuwa ikielekezwa Somalia.

Meli tatu zilikuwa zimebadilisha safari zake ili kusaidia mabaharia katika meli hiyo ya kubeba mizigo mizito, iliyokuwa imetekwa nyara katika ufuo wa Yemen.

Wanamaji kutoka ndege ya Uchina walipanda kwenye meli hiyo iliyokuwa imetekwa na kugundua kuwa maharamia hao walikuwa wametoroka.

Huo ulikuwa utekaji nyara wa tatu kwa muda wa majuma machache yaliyopita.