Kwa picha: Kimbunga Debbie nchini Australia

Kimbunga kwa jina Debbie kimekumba eneo la kaskazini mashariki mwa jimbo la Queensland na kusababisha mvua kubwa eneo hilo.

Maelfu ya watu wamehamishwa huku wengi wakitafuta hifadhi katika makao ya muda.

Moja ya maeneo yaliyoathiriwa ni la Airlie Beach eneo maarufu kwa watalii ambalo limegeuka na kuwa mahame kufuatia kuwasili kwa kimbunga hicho.

Baadhi ya majengo yaliharibiwa.

Miti mikubwa iling'olewa na upepo mkali wa kimbunga hicho.

Wakaazi wa maeneo karibu na pwani wakiwemo wale walio mji wa Ayr wamehamishwa.

Watoto walibaki nyuma huku shule zikifungwa wakati wa dharura hiyo.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Australia, Jumanne jioni ilionyesha kimbuna eneo la Queensland.

Mtandao unaofuatia hali ya hewa wa WindyTV nao ulionyesha kimbunga hicho.

Siku ya Jamatatu mawingu ya kimbunga hicho yalionekana katika anga ya Ayr.

Picha za Satellite : Australian Bureau of Meteorology.