Fifa yampiga marufuku ya maisha refa raia wa Ghana

Chanzo cha picha, Joseph Lamptey
Refa raia wa Ghana Joseph Lamptey, amapigwa marufuku ya maisha na shirikisho la kandanda Duniani Fifa, baada ya masuali kuibuka jinsi alivyosimamia mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia kati ya Senegal na Afrika Kusini Novemba iliyopita.
Afrika Kusini ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1 lakini Senegal ikalalamika kwa shirikisho la Fifa.
Walisema kuwa Lamptey aliwapa Afrika kusini penalti licha ya naibu refa kuashiria kuwa ingekuwa kona.
Wengi waliuliza maswali kuhusu kona hiyo wakati huo, kikiwmeo kitengo cha michezo cha BBC kilichoripoti kuwa Afrika Kusini iliongoza baada ya panelti hiyo yenye utata.

Chanzo cha picha, AFP








