Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Washambuliaji wa kujitoa mhanga wawaua watu Nigeria
Washambuliaji wa kujitolea mhanga kaskazini mwa Nigeria, wameuwa watu wane, wakiwemo mwanamke na watoto wake wawili.
Watu kama wanane walijeruhiwa katika kijiji, karibu na mji wa Maiduguri.
Msemaji wa polisi, Viktor Isuku alieleza kuwa washambuliaji watatu mwanamume na wanawake watatu, walijilipua kwa mabomu, walipokabiliwa na kundi la wanamgambo watiifu kwa serikali.
Mwanamgambo mmoja pia alikufa katika shambulio hilo.
Maiduguri ndiko lilipoanza kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, ambalo limeuwa watu elfu 15, tangu lilipoanza kupigana dhidi ya serikali ya Nigeria, miaka minane iliyopita.