Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia bado hajaondoka nchini Malaysia hata baada ya kupewa saa 48 kuondoka
Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia anakabiliwa na notisi ya kuondoka nchini humo kufuatia mgogoro kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha Kim Jong nam nduguye wa kambo rais wa Korea kaskazini.
Siku ya Jumamosi balozi Kang Chol alipewa ilani ya saa 48 kuondoka nchini humo.
Mamlaka ya Malaysia imeishtumu Pyongyang kwa kujaribu kuingilia uchunguzi huo.
Korea Kaskazini nayo imekataa ripoti ya upasuaji ambayo inaonyesha kuwa King Jong nam alifariki baada ya wanawake wawili kumpaka sumu aina ya VX aktika uso wake.