Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Adele atangaza kwamba ameolewa
Msanii wa muziki Adele amethibitisha kwamba ameolewa na Simon Konecki baada ya miezi kadhaa ya uvumi.
Mwanamuziki huyo alikuwa jukwaani huko mjini Brisbane Australia akizungumza kuhusu wimbo wake Someone Like You ,wakati aliposema ,''nimeolewa sasa''.
Kumekuwa na uvumi kwamba wawili hao walioana na kwamba Adele alimtaja kuwa mumewe katika tuzo za Grammy.
Adele na Simon wana mtoto mmoja pamoja-mvulana wa miaka 4 anayejulikana kama Angelo.
Kanda ya video inayomuonesha Adele akizungumza kuhusu ndoa yake imesambazwa katika mitandao ya kijamii.
Alikuwa akielezea wakati alipoimba wimbo ''Someone Like You'' kwa familia yake na marafiki aliposema kwamba ''ameolewa''.
''Niliona katika macho yao wakati walipokuwa wakisikiza kwamba ilikuwa ikiwakumbusha kuhusu kitu ama mtu''.