Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Magufuli amteua Salma Kikwete mbunge
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mama Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Salma ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.