Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
SnapChat yapanda thamani ulimwenguni
Kampuni inayomiliki mtandao wa huduma za ujumbe wa SnapChat imepanda thamani baada ya kuuza hisa zake kwa wawekezaji wakubwa kutoka mjini New York na kufanikiwa kunyakua kitita cha dola bilioni ishirini na nne.
Kuanzia leo SnapChat, itakuwa na uwezo wa kuanza biashara ya hisa.
Kampuni hiyo imejichoma katika soko la hisa la Wall Street ambalo ni kubwa na kulingana na makampuni ya teknolojia, SnapChat ni ya pili kitanguliwa na Facebook iliyoundwa mwaka 2012.
Katika kipindi cha miaka mitano, SnapChat imefanikiwa kuwa kifaa cha majaribio kilichoundwa na wanafunzi wawili wajishughulishao na masuala ya mitandao ya kijamii yenye watumiaji laki moja na elfu sitini ulimwenguni kote.