Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uganda yazindua mpango kusaidia wanawake tasa
Uganda imezindua mpango wa kuwasaidia wanawake wagumba kukabiliana na unyanyapaa.
Wanawake wengi wasioweza kupata watoto wanasema wanapitia mengi yakiwemo waumezao kuwafukuza kutoka majumbani mwao kwa sababu ya ugumba.
Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango anasema inakadiriwa kuwa nchini Uganda kuna wanawake wagumba takriban millioni tano, kwa mujibu wa waziri wa taifa wa afya Bi Sarah Opendi.
Kawaida wanawake hawa hulaumiwa kwa tatizo hilo sugu japo waziri anasema huenda shida iko kwingine.
Bi Opendi anasema kuwa tatizo hili linaathiri wanawake kati ya asilimia 10 na 15, na kuongeza kuwa uchunguzi uliofanywa unamatokeo ya kusisimua.
Waziri ametoa kauli hiyo wakati wa kuzindua mpango utakao wasaidia wagumba wa Uganda kujitosheleza kimaisha baada ya kunyanyashwa.
"Uzinduzi wa mpango huu utakuwa na manufaa mengi kama anavyofafanua," anasema mmoja wa wanawake waliohudhuria.
Waziri amesisitiza kuwa wanawake wengi hawajui kuwa shida ya kutozaa sana sana ni ya wanaume na hivyo baadaye wengi wakifahamu hilo hawatakubali kunyanyaswa na kufukuzwa kutoka nyumbani kwao eti kwa sababu wameshindwa kuzaa.