Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanaharakati anayeshukiwa kupewa sumu Urusi apelekwa matibabu ng'ambo
Mwana harakati wa Urusi, Vladimir Kara Murza, ameondoka nchini baada ya kulazwa hospitali kwa zaidi ya majuma mawili, akiwa mahututi.
Inashukiwa kuwa mwana harakati huyo alipewa sumu.
Karatasi za hospitali zinasema aliugua kutokana na kitu kisichojulikana.
Alisafirishwa kwa ndege kutoka Urusi, akifuatana na mkewe na tabibu, kuenda kuendelea kutibiwa nchi za nje.
Taarifa ilisema kuwa Bwana Kara Murza, ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa kiongozi wa upinzani aliyeuwawa, Boris Nemtsov, anakusudia kuendelea na kazi yake ya kurejesha demokrasi nchini Urusi.