Madona aruhusiwa kupanga watoto 2 kutoka Malawi

Mahakama ya juu nchini Malawi imemruhusu mwanamuziki raia wa Marekani Madona, kupanga watoto wawili kutoka nchini humo, kwa mujibu wa shirika la Reuters.

Mwezi uliopita mwanamuziki huo wa nyimbo za Pop alikana madai kuwa alikuwa ametuma maombi ya kutaka kupanga watoto wawili zaidi kutoka nchi hiyo ya kusini mwa bara la Afrika.

Inaripotiwa kuwa Madona alikuwa mahakamani mjini Lilongwe wakati jaji alimpa ruhusa ya kupanga watoto wawili zaidi.