Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Serikali ya Syria yakana kuwa Bashar al Assad anaugua
Serikali ya Syria imekana taarifa kuwa Rais Bashar al-Assad anaugua, ikisema ni uvumi mtupu unaotumiwa na maadui wa Assad kujaribu kuwapa motisha wanamgambo na waasi waliokata tamaa.
Akisisitiza kuwa Asaad yu buhari wa afya na kwamba anaendelea na kazi zake kawaida, Wameshtumu wapinzani kwa kile wanachokitaja kuwa kutumia propaganda.
Waasi hao wamedaiwa kueneza taarifa ghushi kwamba Bashar amepata mshutuko wa moyo au ana maradhi ya kiakili baada ya miaka sita ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.