Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Theresa May ziarani Marekani, ataka ushirikiano
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema ni wakati sasa nchi yake na Marekani kuanza tena upya mahuasiano yao maalum na majukumu ya kuongoza pamoja katika kipindi hiki.
Akizungumza mjini Philadelphia, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake nchini Marekani, ambayo itamuwezesha pia kuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Donald Trump.
Amesema kwa uhakika nchi yake ambayo imemaliza uanachama wake kwenye Umoja wa Ulaya, iko tayari kujenga ushirikiano na marafiki zake wa zamani na wapya pia.