Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamitindo mwenye jinsia mbili
Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili.
Gaby mwenye umri wa miaka 28 anasema kuwa ameamua kutangaza jinsia yake ili kuhamasisha watu kuhusu watu wenye jinsia mbili mbali na kutoa hamasa kwa jamii.
Ni miongoni mwa wanamitindo wa hadhi ya juu kuzungumzia kuhusu jinsia yake.
Watu wenye jinsia mbili hawana viungo vya ndani ama vya nje vinavyowatambulisha moja kwa moja kuwa na jinsia ya kiume ama ile ya kike.
''Nimefikia wakati katika maisha yangu ambapo nimeamua kutangaza jinsia yangu'', alisema Hanne.
''Ni wakati wa watu wenye jinsia mbili kujitokeza, kuondoa uoga na kuzungumzia maswala ambayo yalitukumbuka tukiwa watoto''.
Hanne ameshiriki katika kuuza mitindo ya Chanel na Prada na pia amekuwa katika kampeni za Mulberry na Balenciaga.
Katiika kanda za video zilizochapishwa katika mtandao wake wa Instagram ,anaelezea kwamba licha ya kuzaliwa na jinsia mbili hajashindwa kupigania kazi yake katika sekta ya mitindo.