Donald Trump amfananisha mwanamke na mwanawe kimakosa mtandaoni

Mwanamke mmoja kutoka Brighton nchini Uingereza aliyefananishwa kimakosa na mwana wa kike wa Donald Trump, Ivanka Trump katika mtandao wa Twitter na rais huyo mteule wa Marekani mwenyewe ameambia BBC kwamba siku yake ilianza na mshangao mkubwa.

Ivanka Magic ambaye ni mshauri wa maswala ya kidijitali alisema yeye na mumewe waliamshwa saa kumi na mbili asubuhi kutoka kwa simu za baadhi ya vyombo vya habari.

Ujumbe wa Twitter uliochapishwa na Donald Trump

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Ujumbe wa Twitter uliochapishwa na Donald Trump

Vilimwambia kwamba alishiriki katika mazungumzo ya Twitter na Donald Trump yalioshirikisha wafuasi wake milioni 20.

Bw Trump alikuwa akimsifu mwanawe kwa kutumia jina la mtu mwengine kimakosa.

Ujumbe wa Twitter uliochapishwa na Ivanka Magic akimjibu Donald Trump

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Ujumbe wa Twitter uliochapishwa na Ivanka Magic akimjibu Donald Trump

Watumiaji hatahivyo waliingilia kati kwa haraka na kukosoa makosa hayo.

Naye bi Magic akajibu: Bi Magic ambaye amekuwa akikifanyia kazi chama cha Leba awali alisema kuwa aligundua kilichofanyika baada ya chombo kimoja cha habari kumtumia ujumbe mumuwe.

Ivanka Trump ,mwanawe Donald Trump
Maelezo ya picha, Ivanka Trump ,mwanawe Donald Trump

''Nilishuka hadi chini kuangalia simu yangu na nilipata jumbe nyingi, aliambia BBC.Sio jambo la kawaida kuzungumzia kuhusu ITV na BBC ndani ya dakika 45 za kuamka kwako''.

Ivank Magic aliyefananishwa kimakosa na mwanawe Ivank Trump, mwana wa kike wa rais mteule wa Marekani Donald Trump

Chanzo cha picha, Ivan Magic

Maelezo ya picha, Ivank Magic aliyefananishwa kimakosa na mwanawe Ivank Trump, mwana wa kike wa rais mteule wa Marekani Donald Trump

Jina la utambulisho linalotumiwa na bi Ivanka kuingia katika kompyuta yake ni@Ivanka na lile la mwanawe Trump ni @Ivanka Trump.

Amesema kuwa amekuwa akifananishwa kimakosa na mwana wa Trump katika mtandao wa Twitter kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita lakini sio kwa kiwango hicho.