Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waandamana kupinga uwindaji wa tembo Tanzania
Takriban watu 500 wameandamana katika mji mkubwa nchini Tanzania Dar es Salaam kupinga uwindaji wa tembo.
Maandamano hayo ya kilomita 5 yalianza katika ubalozi wa China mjini humo.
Takriban tembo 30,000 huuwawa kila mwaka barani Afrika na soko kubwa la pembe za ndovu ni China.
Mwishoni mwa mwezi Disemba Beijing ilitangaza kwamba itapiga marufuku biashara ya pembe za ndovu kuanzia mwisho wa mwaka huu.
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya Afrika yalioathirika sana na uwindaji haramu wa tembo huku utafiti ukibaini kwamba idadi ya wanyama hao imepungua kwa asilimia 60 kati ya 2009 na 2014.