Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Omar el Bashir afanyiwa uchunguzi wa moyo
Rais wa Sudan Omar El Bashir amefanyiwa ukaguzi wa moyo katika hospitali kuu mjini Khartoum.
Taarifa kutoka chombo cha habari cha serikali, Suna imesema kuwa rais huyo mwenye umri wa miaka 73 amefanyiwa uchunguzi wa moyo ambao hufanyika kutibu magonjwa ya moyo katika hospitali ya Royal Care siku ya Jumatano.
Hatahivyo chombo hicho kinasema kuwa ataendelea na kazi zake rasmi.
Chombo cha habari cha Reuters kilijadiliana na afisa mmoja wa serikali aliyesema kuwa matokeo ya uchunguzi huo yalimpatia motisha, kikiongezea kuwa rais aliondoka mara moja baada ya matibabu hayo.
Bwana Bashir alichukua madaraka mwaka 1989 katika mapinduzi na ameiongoza Sudan tangu wakati huo.
Ameshtumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuvifungia vyombo vya habari hatua ambayo imesababisha maandamano katika siku za hivi karibuni.
Bashir anatafutwa na mahakama ya ICC kwa mashtaka ya mauaji ya halaiki ya watu, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu, madai anayokana.
Ameambia BBC mwaka uliopita kwamba atajiuzulu mwisho wa muhula wake 2020.