Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waziri wa habari Gambia akimbilia Senegal
Waziri wa habari nchini Gambia Sheriff Bojang amekimbia kwenda Senegal ikiwa ni ishara kuwa Rais Yahya Jammeh, anakabalia na upinzani kutoka ndani ya baraza lake la mawaziri baada ya kukataa kuachilia madaraka wakati kipindi chake kitakapofika ukingoni tarehe 19 mwezi huu.
Bwana Bojang alisema kwenye taarifa kuwa uamuzi wa Jammeh wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa Disemba mosi, ni hatua ya kuzima matwakwa ya watu wa Gambia.
Ametoa ushauri kwa mawaziri wengine wajiuzulu kutoka kwa serikali ya Jammeh ya miaka mingi.
Gazeti mmoja linalounga mkono upinzani nchini Gambia linasema kuwa Bojang aliwasili kwenye mji mkuu wa Senegal Dakar siku chache zilizopita na hana nia ya kurudi Gambia tena.
Bwana Bojang alitambuliwa kuwa mwendesha propaganda mkubwa wa bwana Jammeh ambaye wakati wingi alikuwa akionekana kwenye vyombo vya habari akisoma taarifa zenye utata za serikali.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Neneh Macdouall Gaye, alijiuzulu mwezi uliopita licha ya hatua yake kupata umaarufu kidogo.
Kiongozi wa upinzani Adama Barrow ambaye alimshinda bwana Jammeh kwenye uchaguzi alisema kuwa atajitangaza rais tarehe 19 mwezi huu.