Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanadiplomasia wa Urusi waliofurushwa Marekani waondoka
Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti kuwa wanadiplomasia 35 wa Urusi waliofurushwa na rais Barack Obama kutoka Marekani wameondoka wakiandamana na familia zao .
Urusi ilituma ndege maalum ya kuwarudisha nyumbani.
Wanadiplomasia hao waliamuriwa kuondoka Marekani baada ya Urusi kushtumiwa kuwa ilijaribu kuingilia uchaguzi wa hivi majuzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.
Vyombo vya kijasusi vya Marekani vinadai kuwa utawala wa Urusi ndio ulioamuru kudukuliwa kwa hasa tovuti ya chama cha Democratic ili kuvuruga kapeni za bi Clinton na kumsaidia Donald Trump ambae sasa ndiye rais mteule.