Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Balozi wa Urusi apigwa risasi na kufariki Uturuki
Balozi wa Urusi aliyepigwa risasi nchini Uturuki Andrey Karlov amefariki.
Balozi huyo alishambuliwa katika eneo la sanaa ya uchoraji katika mji mkuu wa Ankara.
Ripoti zinasema kuwa balozi huyo alikuwa akitoa hotuba wakati mtu aliyekuwa amejihami na bunduki alipompiga risasi na kutoa ujumbe kuhusu mji wa Aleppo nchini Syria.
Watu kadhaa wamejeruhiwa .Picha za tukio hilo zimewaonyesha watu wawili waliovalia nadhifu wakilala ardhini ,karibu na kipaza sauti.
Uturuki na Urusi zimekuwa zikizozana kuhusu kujihusisha kwao nchini Syria.
Kumekuwa na maandamano nje ya ubalozi wa Urusi mjini Istanbul katika siku za hivi karibuni kuhusu hatua ya Urusi kuunga mkono serikali ya Syria.
Lakini serikali za Uturuki na Urusi zimekuwa zikishirikiana katika usitishwaji wa vita huko Aleppo.