Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
EU yatoa mamilioni ya dola kudhibiti wahamiaji Niger
Umoja wa Ulaya umetoa dola zaidi ya milioni sita kwa Niger kwa ajili ya kukabiliana na wahamiaji wanaotumia mipaka ya nchi hiyo kuelekea Ulaya.
Ukanda wa jangwa wa Agadez nchini Niger hutumika kama njia kuu ya wahamiaji kuelekea nchini Libya na kisha kutumia bahari ya Mediterranea kuingia Ulaya.
Mpango kama huo umekwisha fanyika kwa nchi kama Senegal, Ethiopia, Nigeria na Mali na umoja wa Ulaya unapanga kutafuta nchi nyingine zaidi za Afrika kuweza kusaidia suala hilo.