Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamke ajifungua kwa kutumia tishu za ovari za utotoni
Mwanamke aliyepata mtoto London kwa kutumia tishu za ovari zilizogandiswa akiwa mtoto ameelezea kuzaliwa kwa mtoto wake kama muujiza.
Inasemekana kuwa hii ni mara ya kwanza kwa madaktari popote ulimwenguni kutumia utaalam kama huo kuweza kupata mtoto.
Madaktari wake wanasema kuwa mafanikio hayo yatatoa matumaini zaidi kwa watoto wengine wenye tishu za ovari zilizohifadhiwa kabla ya kufanyiwa matibabu ya saratani.
Moaza Al Matrooshi,mwenye asili ya Dubai, alizaliwa na matatizo ya mfumo kwenye damu yaliyomfanya asiweze kuzaa akiwa mtu mzima ambapo tishu za ovari zake zilichukuliwa na kuhifadhiwa na wataalam hao wa afya ili kuchanganya na mayai yake atakapokuwa mkubwa kisha kupatikana kwa mtoto.