Zaidi ya watu 100,000 kwenye hatari ya kufa njaa Nigeria

Chanzo cha picha, Save the Children UK
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa zaidi ya watu 100,000 wako hatarini ya kufa kutokana na njaa Katika Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwa sababu ya maasi ya Boko Haram.
Umoja wa Mataifa unasema umeteka nyara sehemu nyingi zilizokuwa zimekaliwa na Boko Haram, lakini ukosefu wa usalama una maana kwamba wakulima hawawezi kuendele na shughuli zao za kupanda.

Chanzo cha picha, Save the Children UK
Umoja wa Mataifa unasema kuwa watu milion Saba wanahitaji msaada wa kibinadamau mara moja.
Umetoa wito kwa msaada wa zaidi ya Dola Bilioni moja kupunguza matatizo ya kibinadamu Barani Afrika hii leo.








