Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Prince Harry akutana na Rihana Barbados
Prince Harry, mwanamfalme wa Uingereza amekutana na nyota wa muziki wa Pop Rihana mara mbili kwa siku katika warsha ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Barbados.
Rihana ambaye muziki wake umebobea nchini Uingereea alisamama na kumsalimia Prince Harry.
Kisha wawili hao wakaketi pamoja jukwaani wakati ya sherehe.
Msaidizi mmoja alisema kuwa Prince Harry ambaye alivalia nguo rasmi za ufalme alisema kuwa Harrry alikuwa amejulishwa dakika 20 kabla awasili kwa warsha hiyo kuwa Rihana angehudhuria.
Baadaye Harry na Rihana tena waliketi pamoja kwenye jukwaa eneo la Kensington huko Bridgetown.
Umati wa watu 20,000 uliohudhuria ulimshangilia Prince Harry wakati jina lake lilipotajwa, Lakini kulikuwa na mbwembwe zaidi wakati jina la Rihana lilitajwa.