Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump alipa dola milioni 25 kumaliza kesi
Wakili wa rais mteule wa Marekani Donald Trump ametatua kesi ya mamilioni ya madola iliyokuwa inamkabili mteja wake ili apate nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya na kuangazia changamoto zinazoikabili Marekani.
Trump alikuwa ameshtakiwa na wanafunzi wa zamani kwa ubadhirifu wa pesa katika chuo kikuu cha Trump,ambapo wanafunzi walilipa maelfu ya madola kwa masomo baada ya kuhadaiwa kwamba watafunzwa siri juu ya uwekezaji
Rais huyo mteule amekuwa akikanusha madai hayo lakini hatimaye ameamua kulipa dola milioni ishirini na tano ili kumaliza kesi hiyo. Mpango huo hata hivyo haumuhitaji kukiri kwamba alifanya makosa.