Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Uvuvi wa pweza Zanzibar
Mchanga mweupe wa bahari kutoka mashariki mwa pwani ya Zanzibar husifika sana kama eneo la mapumziko.
Lakini kila siku, wakati maji yanajaa na watalii wanarudi hotelini, kundi dogo la wanawake na wanaume wakiwa wamebeba fimbo na mishale wanaelekea baharini kutafuta mojawapo ya vyakula vitamu vya kisiwa hicho cha Tanzania - pweza.
Wakati maji yakikupwa mara moja mvuvi wa pweza aliye na ujuzi anaweza kunasa takriban pweza 10 wanaoishi katikati mwa mawe, matumbawe na nyasi za baharini.
Samaki hao wanaouzwa kwa bei ghali katika hoteli za kitalii na huwa na protini ya hali ya juu kwa jamii zinazoishi pwani.
Matumbawe huwa chanzo cha kujikimi maisha kwa wakaazi wa eneo hilo maana hupata samaki kama vile kaa, na pweza.
Pweza wengi hupatikana Tanzania magharibi mwa bahari Hindi.
Abdullah Ali, mwenye umri wa miaka 35, ajitayarisha kuodnoka na boti lake la mbao ili kuwinda pweza kutoka kijiji cha Dongwe.
Hii imekuwa kazi ya wanawake kitamaduni lakini wanaume pia sasa wamejishughulisha na kazi hiyo ya uindaji kutafuta riziki.
"Pweza wamenisaidia kusukuma maisha," anasema Ali, anayejipatia $2.30 kwa kila kilo ya pweza.
Kwa mujibu wa data kutoka shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO, uwindaji pweza umeongezeka Tanzania kutoka tani 482 mnamo 1990 hadi 1,250 mwaka 2012.
Mwamba na mandhari ya bahari yanatoa nafasi kwa pweza kujificha wakati maji yamekupwa baharini, na kufanya vigumu kuonekana kwa mtu asiye na uzoefu.
Mariam, muindaji pweza kutoka kijiji cha Bwejuu village, anazama ndani ya maji kupunguza joto baada ya kazi ya asubuhi.
Mama Juma, muindaji wa pweza, anakagua maji karibu na mwamba wa Paje katika maenoe ambayo huenda pweza wamejificha.
Mwanamke atafuta pweza jioni huko Bwejuu.
Jamii hutegemea samaki hao wa maji madogo kujikimu kimaisha.
Pweza wa kuchomwa ni chakula maarufu kinachouzwa katika soko la samaki usiku Stone Town.
Pweza wengi wanaovuliwa Tanzania bara husafirishwa Ulaya, lakini utalii katika kisiwa cha Zanzibar umetoa soko kubwa.