Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mshukiwa wa shambulio la ugaidi ajiua Ujerumani
Mshukiwa wa shambulizi la bomu huko Ujerumani Raia wa Syria amejiua akiwa garezani.
Jaber Albakr alikutwa kajinyonga akiwa gerezani huko mji wa Leipzig.
Alikabidhiwa polisi siku ya jumatatu na raia mwenake wa Syria baada ya kuwa mafichoni kwa siku mbili, raia huyo alipewa nafasi ya kuishi ujerumani kama zawadi ya kutoa taarifa.
Mwanasheria mtetezi wa Albakrs ameelezea kifo chake kama ni kashfa, amesema kuwa askari magereza walikua wanajua kama ana hatari ya kutaka kujiua.
Albakr alikamatwa baada ya kutafutwa kwa muda mrefu kwa kushukiwa kupanga shambulizi la uwanja wa ndege wa Berlin.
Polisi wanasema walikuta gramu 1.5 ya bomu ndani ya ghorofa yake katika mji wa Chemnitz, pia maafisa usalama wa Ujerumani wamesema walipokea taarifa wiki iliyopita kuwa mshukiwa huyo alikua akitumia mtandao kupata maelekezo ya kutengeza mabomu.