Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Obama: Waliohusika na jaribio la mapinduzi Uturuki kushtakiwa
Rais wa Marekani Barrack Obama anasema kuwa atahakikisha kuwa wale waliohusika na jaribio la mapinduzi nchini Uturuki watashtakiwa.
Alikuwa akizungumza alipokutana na rais Recep Tayyip Erdogan kandokando ya mkutano wa G-20 mjini Hangzhou nchini China.
Uturuki inadai kuwa kiongozi wa dini mwenye makao yake huko Marekani Fethullah Gulen ndiye aliyepanga njama ya mapinduzi hayo na inataka arudishwe nchini Uturuki.
Lakini rais Obama hakuzungumzia kuhusu swala la kumrudisha Uturuki kiongozi huyo.
Bwana Gulen amekana kuhusika na jaribio hilo.Rais Obama na Erdogan pia walizungumzia kuhusu hali ilivyo nchini Syria.