Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Viongozi wa upinzani wa Chadema nchini Tanzania kuhojiwa zaidi na polisi
Viongozi wa chama cha upinzani cha Chadema Nchini Tanzania walioshikiliwa jana jioni na kuhojiwa na jeshi la polisi na baadaye kuachwa kwa dhamana, wanatarajiwa kurudi tena kikuo kikuu cha polisi leo kwa maojiano zaidi.
Viongozi hao walikamatwa jana jioni wakiwa kwenye Hoteli ya Girrafe iliyopo mjijini Dar es salaaam wakifanya mkutano wa ndani ya chama hicho.
Kupanga mikakati ya kutekeleza kile wanachokiita Operasheni Ukuta.
Inayotarajiwa kufanyika septemba mosi ikilenga kupinga kile wanachokiita ni kubanwa kwa demokrasia kwa serikali ya awamu ya tano.
Polisi waliwashikilia viongozi hao kufuatia kukiuka amri iliyotolewa na jeshi la polisi mwishoni mwa juma lililopita kupiga marufuku mikutano yote ya ndani ya vyama vya siasa.
Kufuatia mauaji ya askari polisi wanne yaliyotokea nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Waliokamatwa ni mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, katibu mkuu Dk. Vicent Mashinji, naibu Katibu mkuu bara John Mnyika na makamu mwenyekiti Zanzibar Said Issa.