Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uingereza kupambana na unene wa kupindukia kwa Watoto
Mpango wa kupambana na unene wa kupindukia kwa watoto nchini Uingereza utatangazwa Alhamisi,mpango huo una nia ya kupunguza Sukari kwenye Vyakula na vinywaji kwa 20% kwa kipindi cha miaka zaidi ya minne.BBC imeelezwa.
Lakini hatua hizo hazihusishi kuzuia matangazo ya vyakula kwenye Televisheni.
Vyanzo vya habari vinasema mpango huo utaeleza pia kuhusu masuala ya Kodi kwa vinywaji vyaenye sukari.
Mipango ya kupambana na tatizo hilo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kwa miezi kadhaa.