Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanajeshi wa AU waliouza mafuta Somalia wafungwa
Walinda amani tisa wa Muungano wa Afrika wamefungwa jela kwa kushiriki katika bishara ya uuzaji mafuta nchini Somalia.
Wanajeshi hao ambao wote ni kutoka nchini Uganda, wamehukumiwa vifungo vya kati ya mwaka moja na miaka mitatu na mahakama ya kijeshi ya Uganda.
Watatu kati ya wanajeshi hao pia wamefutwa kutoka jeshini.
Hii ndiyo mara ya kwanza mahakama ya kijeshi ya Muungano wa Afrika, imefanya kikao nchini Somalia tangu wanajeshi hao wapelekwe nchini humo miaka tisa iliyopita.
Uganda ndiye mchangiaji mkubwa wa wanajeshi wa kikosi cha wanajeshi 22,000, kinachopigana na wanamgambo nchini Somalia.