Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sudan Kusini yakubali walinda amani zaidi
Serikali ya Sudan Kusini imekubali kuruhusu kikosi chengine cha kuweka amani kujaribu kuokoa mkataba wa amani,kulingana na shirika la Igad.
Vita vya kikabila mwezi uliopita viliwawacha takriban watu 300 wakiwa wamefariki na nusra vizuwe vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimewaua makumi ya maelfu ya watu.
Wanajeshi 12,000 wa Umoja wa Mataifa walishindwa kuzuia shambulio hilo.
Hakuna siku maalum ya wanajeshi wa Umoja wa mataifa kuingia nchini humo na Sudan Kusini haijathibitisha tangazo hilo la Igad.
Rais Salva Kiir amekuwa akipinga mpango huo wa vikosi zaidi kuingia nchini humo.