Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Liverpool yakataa ofa za Doak

Muda wa kusoma: Dakika 3

Liverpool wamekataa ofa ya pauni milioni 15 kutoka kwa Crystal Palace kwa ajili ya kumnunua Ben Doak. Kiungo huyo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 19 yuko kwa mkopo Middlesbrough . (Tme - subscription required)

Liverpool wanataka pauni milioni 30 ikiwa wanataka kumuuza kinda Doak. (Independent)

The Reds pia wamekataa dau la pauni milioni 16 kutoka kwa Ipswich kwa ajili ya Doak na wangependelea abaki Middlesbrough hadi mwisho wa msimu. (subscription required

Arsenal wanachunguza uhamisho wa Januari wa kumnunua mshambuliaji wa Wolves wa Brazil Matheus Cunha, 25. (Football Insider)

Wolves wanafanyia kazi mkataba mpya Cunha ili kujaribu kumbakisha klabuni hapo. (Mirror)

Ofa ya Crystal Palace ya pauni milioni 12.4 ya kumnunua beki wa Senegal mwenye umri wa miaka 20 El Hadji Malick Diouf ilikataliwa. ( Mercato Foot)

Newcastle wanatazamiwa kupata faida kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano lakini bado wanapaswa kuuza wachezaji kabla ya kununua mwezi huu ikiwa watafuata sheria za kifedha za Primia Ligi. (Subscription required)

Napoli wameonyesha nia ya kutaka kumsajili winga wa Chelsea Muingereza mwenye umri wa miaka 18 Carney Chukwuemeka, ambaye thamani yake ni takriban £30m. (TeamTalk)

Manchester City wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa Lens wa Uzbekistan Abdukodir Khusanov, 20. (Telegraph - subscription required)

Klabu ya Saudi Pro League Al - Shabab ina uhakika wa kufikia makubaliano ya kumnunua kiungo wa kati wa Wolves '31 wa Gabon Mario Lemina. (Rudy Galetti)

Winga wa Brentford Muingereza Keane Lewis-Potter, 23, anakaribia kukubaliana na mkataba mpya. (Subscription required)

Wolves wanatumai kukamilisha usajili wa pauni milioni 15 wa beki wa kati wa Reims , 27 wa Ivory Coast Emmanuel Agbadou mapema wiki ijayo. (Telegraph),

Klabu ya Uturuki Trabzonspor inamtaka mshambuliaji wa Southampton Paul Onuachu lakini wako tayari kulipa £4.2m pekee. The Saints wanataka £8.3m kwa Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 30. (Gunebakis - in Turkish)

St Johnstone wanataka kumsajili beki wa kulia wa Liverpool na Scotland Calvin Ramsay, 21, kwa mkopo baada ya muda wake wa mkopo Wigan kupunguzwa. (Courier)

Leeds United wako tayari kuwasilisha zabuni kwa kiungo wa kati wa Coventry City Muingereza Ben Sheaf, 26, mwezi Januari. Wapinzani wao wa ubingwa wangependa sikiliza ofa zaidi ya £8m. (Leeds United News)

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi