Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Real Madrid tayari kumgharamia Alexander-Arnold

Muda wa kusoma: Dakika 3

Real Madrid wako tayari kulipa Liverpool ada ya kumsajili beki wa kulia wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26, kabla ya Kombe la Dunia la Klabu mwezi Juni. (Sun)

Arsenal wanaongoza Tottenham katika mbio za kumnunua mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 21, kutoka RB Leipzig . (Football Insider)

Mshambulizi wa Uswidi Viktor Gyokeres, 26, ameonyesha nia yake ya kuondoka Sporting msimu huu wa kiangazi. (Rekord - in Spanish

Liverpool na Arsenal zinaweza kumudu kumsajili Alexander Isak, 25, msimu wa kiangazi bila kukiuka sheria za kifedha, licha ya Newcastle kumthamanishwa mshambuliaji huyo wa Uswidi kwa pauni milioni 150. (Football Insider)

Liverpool wamedhamiria kumsajili beki wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez, 21, kutoka Bournemouth msimu wa kiangazi, huku Real Madrid pia wakiangalia uwezekano wa kumnunua. (TeamTalk)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 19, ana nia ya kukataa ofa ya kandarasi mpya kutoka kwa Manchester United na kuhamia nje ya nchi, huku klabu ikiwa tayari kumuuza kwa takriban £70m. (Guardian)

Harry Kane anaweza kurejea kwenye Ligi ya Primia msimu huu huku Bayern Munich wakifikiria kumruhusu mshambuliaji huyo wa Uingereza, 31, kuondoka ikiwa klabu itatimiza masharti yake ya pauni milioni 67. (Sun)

Newcastle inaweza kumsajili fowadi wa Porto na Uhispania Samu Aghehowa kwa dau la chini zaidi kuliko kifungu chake cha pauni milioni 82.5 msimu huu wa kiangazi, huku Arsenal , Aston Villa na West Ham zikifikiriwa kufuatilia hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Football insider)

Liverpool wana nia ya kutaka kumnunua kiungo wa Stuttgart na Ujerumani Angelo Stiller, 23. (Bild via Daily Briefing - in Germany )

Manchester United wanatafuta kwa bidii nafasi za kuachana na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 33, ambaye anataka kuwa zaidi ya mchezaji asiye na uwezo. (TeamTalk)

Mshambuliaji wa Canada Jonathan David, 25, ana nia ya kuhamia Uingereza msimu huu wa joto wakati kandarasi yake itakapoisha Lille , huku Manchester United , Tottenham , Chelsea na Newcastle zote zikivutiwa. ((Caught Offside))

Juventus wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Atalanta wa Brazil Ederson, 25, fowadi wa Nigeria Ademola Lookman, 27, na mshambuliaji wa Italia Mateo Retegui, 25. (La Gazzetta dello Sport - in Italian).

Juventus wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Atalanta wa Brazil Ederson, 25, mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, na mshambuliaji wa Italia Mateo Retegui, 25. (La Gazzetta dello Sport - in Italian).

Manchester City wamekubali kulipa Pauni 235,000 za Hibernian kwa mlinda mlango wao wa shule ya Scotland, Ben Vickery, 15. (Manchester Evening News).

Imetafiriwa na Dinah Gahamanyi