Roe v Wade: Kliniki za utoaji mimba zimeanza kufungwa baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu

Kliniki zimeanza kufungwa katika baadhi ya majimbo ya Marekani baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu siku ya Ijumaa kuondoa haki ya kikatiba ya wanawake wa Marekani ya kutoa mimba.
Takriban nusu ya majimbo yanatarajiwa kuanzisha vikwazo vipya au marufuku baada ya mahakama kubatilisha uamuzi wake wa miaka 50 wa Roe v Wade.
Kati ya majimbo hayo, 13 imeharamisha uavyaji mimba papo hapo.
Rais Joe Biden alielezea uamuzi huo kama ‘’kosa la kusikitisha’’.
Maandamano yanaendelea katika miji kote Marekani.
Huko Phoenix, Arizona, polisi walirusha gesi ya kutoa machozi baada ya waandamanaji wanaounga mkono kugonga milango na madirisha ya makao makuu ya serikali.
Huko Los Angeles waandamanaji walizuia kwa muda msongamano wa magari kwenye barabara kuu.
Katika kliniki ya uavyaji mimba huko Little Rock, Arkansas - jimbo lililo na kile kinachojulikana kama sheria ya kuchochea kuruhusu kupiga marufuku papo hapo - milango ya eneo la wagonjwa ilifungwa mara tu maoni ya mahakama yalipowekwa mtandaoni na kilio kilisikika.
Wafanyikazi walipiga simu kuwaambia wanawake kwamba miadi yao imefutwa.
‘’Haijalishi jinsi tunavyojitayarisha kwa habari mbaya, hatimaye inapofika, inapiga sana. Kuwapigia simu wagonjwa hawa na kuwaambia kuwa Roe v Wade imepinduliwa ni jambo la kuhuzunisha,’’ muuguzi Ashli Hunt aliambia BBC.Wasindikizaji katika zahanati hiyo, ambao walisimama juani huko Arkansas baada ya kuandamana na wagonjwa kupitia umati wa waandamanaji, walikumbatiana kwa pamoja.
‘’Nilifikiri kwamba nchi hii bado ingejali watu. Bado ingejali wanawake,’’ alisema Bi Karen, msindikizaji mkuu alisema.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Nje, waandamanaji wa kupinga uavyaji mimba walisherehekea.
‘’Tunasherehekea juu ya taarifa!’’ Alifokea waandamanaji akiwaelekeza watu ambao bado wanaegesha magari yao kwenye zahanati hiyo ambao walikuwa bado hawajasikia kuhusu uamuzi huo.
‘’Pendekezo langu ni kwa wewe kugeuka na kuondoka mahali hapa pa dhambi, mahali hapa pa ukosefu wa haki, mahali hapa pabaya.’’
Huko New Orleans, Louisiana - jimbo lingine la sheria - Kituo cha Huduma ya Afya ya Wanawake, mmoja wa watoa mimba watatu tu katika jimbo hilo, kilifungwa na wafanyikazi wake walikuwa wamekwenda nyumbani.
Nje ya kliniki, msindikizaji wa kujitolea Linda Kocher aliambia BBC kwamba wanawake matajiri bado wataweza kutoa mimba katika majimbo mengine lakini ‘’wanawake maskini wataishia kwenye uchochoro’’ kwa taratibu zisizo halali.
Lakini mwanaharakati wa kupinga uavyaji mimba Mchungaji Bill Shanks alisema ilikuwa ‘’siku ya kusherehekea.’’
Kwa ujumla, uamuzi wa Mahakama ya Juu unatarajiwa kumaanisha wanawake wapatao milioni 36 walio katika umri wa kuzaa watapoteza fursa ya kutoa mimba katika majimbo yao, kulingana na utafiti kutoka Planned Parenthood, shirika la afya linalotoa mimba.
- Sheria za kuchochea huko Kentucky, Louisiana, Arkansas, Dakota Kusini, Missouri, Oklahoma na Alabama tayari zimetumika
- Marufuku huko Mississippi na North Dakota itaanza kutekelezwa baada ya mawakili wao wakuu kuidhinisha
- Marufuku ya Wyoming itaanza kutekelezwa ndani ya siku tano, marufuku ya Utah ilazima iidhinishwe na baraza la sheria
- Marufuku huko Idaho, Tennessee na Texas iatumika baada ya siku 30.
‘’Kila maisha ya binadamu yanahitaji kulindwa,’’aliambia BBC huku akimtazama Bw Biden akikosoa uamuzi wa Mahakama ya Juu.
‘’Inawakilisha kwamba tunakubali ubinadamu wa watoto ambao hawajazaliwa.’’
Bw Biden alisema uamuzi huo unaweka afya ya wanawake na maisha hatarini.
‘’Ni utambuzi wa itikadi kali na makosa ya kutisha ya Mahakama ya Juu,’’ alisema.

Pia unaweza kusoma:
Alisema atafanya kazi kuhakikisha kuwa viongozi wa serikali na serikali za mitaa hawawezi kuzuia wanawake wanaosafiri kwenda kutoa mimba katika majimbo ambayo utaratibu huo ni halali, na pia atalinda upatikanaji wa wanawake wa uzazi wa mpango na dawa za kukomesha mimba hadi wiki 10 ambazo hutumika kutibu kuharibika kwa mimba.
Uamuzi wa Ijumaa ni sawa na ubadilishaji wa jumla wa mfano wa kisheria wa Mahakama ya Juu - hatua adimu sana - na kuna uwezekano wa kuanzisha vita vya kisiasa ambavyo vitagawanya taifa.
Magavana wa majimbo ya pwani ya magharibi California, Washington na Oregon wameapa kuwalinda wagonjwa wanaosafiri kutoka majimbo mengine kwa ajili ya kuavya mimba.
Katika majimbo ambapo maoni kuhusu uavyaji mimba yamegawanywa kwa karibu - kama vile Pennsylvania, Michigan na Wisconsin - uhalali wa utaratibu unaweza kubainishwa kwa misingi ya uchaguzi baada ya uchaguzi.
Katika nyinginezo, uamuzi huo unaweza kuanzisha awamu mpya ya vita vya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuhusu iwapo watu binafsi wanaweza kwenda nje ya nchi ili kutoa mimba au kuagiza dawa za kutoa mimba kupitia huduma za barua.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence, mkosoaji wa muda mrefu wa Roe v Wade, aliwataka wanaharakati wa kupinga uavyaji mimba kutokoma hadi ‘’utakatifu wa maisha’’ utakapolindwa na sheria katika kila jimbo.












