Charles asifu utawala wa Malkia baada ya kutangazwa rasmi Mfalme

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfalme aliahidi kuhudumia taifa kwa "kujitolea bila kuyumba'' sawa na alivyofanya hayati Malkia

Charles III ametangazwa rasmi kama mfalme katika hafla ya kihistoria katika kasri la St James Jumamosi asubuhi.

Bendera zilizoshushwa katika kumuomoboleza Malkia, zitapandishwa juu kikamilifu baada ya hafla hiyo ya baraza la kumtangaza rasmi mfalme, hafla itakayopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni kwa mara ya kwanza.

Mfalme Charles III amepongeza "utawala usio na mithili" wa Malkia baada ya kutangazwa rasmi Mfalme kwenye hafla iliofanyika kwenye kasri la St James. Charles Philip Arthur George ametangazwa rasmi ni Mfalme Charles III. Alipokewa wadhifa huo kufuatia kifo cha mamake Malkia Elizabeth II lakini mkutano wa baraza maalum umemthibitisha rasmi Jumamosi. Ameidhinisha pia siku ambayo mazishi ya Malkia yatakuwa kutangazwa siku kuu licha ya kwamba haijajulikana mazishi ni siku gani hasaa. Akizungumza mbele ya baraza lililomtangaza Mfalme, Charles amesema kifo cha mamake ni "pengo lisilojazika". Wakati huo huo mawaziri wakuu katika bunge la wawakilishi, akiwemo Waziri mkuu Liz Truss wamekula kiapo kwa Mfalme mpya.Charles alipokea Ufalme punde tu baada ya kifo cha mamake Malkia Elizabeth II, lakini kikao rasmi cha kihistoria kilithibitisha jukumu lake Jumamosi. Baraza la kumtangaza rasmi Mfalme, linajumuisha wanasiasa wakuu, majaji na maafisa wengine walimtangaza rasmi kama mfalme. Ni mara ya kwanza hafla hii inapeperushwa kwenye televisheni.

Matangazo mengine yatatolewa rasmi kote Uingereza mpaka Jumapili, wakati bendera zitarudi kupepea nusu mlingoti.

Wakati hafla hiyo ikianza Mfalme mwenyewe hakuweko, lakini alihudhuria awamu ya pili ya shughuli hiyo ya kikao chake cha kwanza cha baraza kuu. Karani wa baraza hilo Richard Tilbrook alitangaza Charles "Mfalme, kiongozi wa jumuiya ya madola, mlinzi wa imani", kabla ya kutangaza "God Save the King" yaani Mungu mlinde mfalme. Chumba kilichojaa watu akiwemo Malkia – mkewe mfalme, mwanamfalme wa Wales na Waziri mkuu Liz Truss, waliiregelea kauli hiyo. Akitoa tangazo lake mwenyewe, Mfalme alisema: "Waheshimiwa, wake kwa waume, ni kwa wajibu na huzuni nawatngazia kifo cha mamangu mpendwa, Malkia.

"Nafahamu jinsi nyinyi, taifa zima na nadhani naweza kusema dunia nzima imehuzunika pamoja nami kwa kuondokewa huku. "Ninafarijika pakubwa kwa risala za wengi kuelezea huzuni kwa dadangu na kaka zangu.

"Na kwamba mapenzi mengi haya na kututia moyo yaifikie familia yetu yote kwa kuondokewa kwetu."

Haya yanajiri baada ya Mfalme kuahidi kumfuata, kipenzi mamake kujitolea maisha kuhudumia katika hotuba yake ya kwanza iliojaa huzuni.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Siku ya Ijumaa ameliambia taifa khusu huzuni mkubwa alio nao, kwa kumpoteza mamake, akisifia mzaha, ukarimu wake na ‘uwezo wake wa kuona wema katika kila mtu’.

Mfalame ameahidi kulitumikia taifa kwa uwajibikaji usiotetereka kama aliokuwa nao mamake Malkia katika utawala wake wa miaka 70.

Charles alikuwa mfalme punde tu mama yake alipofariki, lakini baraza hilo la wakuu wanaomtangaza rasmi hufanyika ounde baada ya kifo cha mfalme kutoa tangazo hilo la mrithi wa kiti cha enzi.

Katika baraza hilo Mfalme atatoa tangazo binafsi kuhusu kifo cha Malkia na kula kiapo kulihifadhi kanisa la Uskotchi – kwasababu kuna mgawanyiko wa sheria kati ya kanisa na serikali.

Miongoni mwa watakaohudhuria hafla hii ni Camilla, mkewe Charles waliooana kwa miaka 17 mpaka sasa ambaye sasa amepokea wadhifa wa Malkia mkewe mfalme, na mwanamfalme mpya wa Wales, William.

Tangazo la kwanza linatarajiwa kutolewa katika roshani ya Friar Court ya kasri la St. James mjini London saa tano saa za huko, muda unaoambatana na mbwembwe za wapiga tarumbeta, milio ya bunduki zinazofyetuliwa kwa heshima katika bustani ya Hyde na katika Jumba refu maarufu la London Tower.

Licha ya kwamba sio sehemu ya shughuli hiyo rasmi ya kutangazwa mfalme, maneno "Malkia amefariki, Mflame aishi Maisha marefu" mara nyingi hutamkwa baada ya hapo.

Siku ya Ijumaa, Charles alikutana na umati wa watu waliopiga kelele "God save the King!" yaani Mungu mlinde Mfalme wakati akisalimiana na umati uliokuwepo nje ya kasri la Buckingham.

Baada yah apo alitoa hotuba kwenye televisheni akieleza matumaini kwamba Mwanawe William kama Mwanamfalme mpya wa Wales na mkewe Catherine - "wataendelea kuwatia watu moyo na kuongoza mdahalo wa kitaifa".

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kutawazwa kwa mfalme kutafanyika katika jini la London la laRoyal Exchange, kwani mama yake alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 70

Tangazo la kwanza linatarajiwa kutolewa katika roshani ya Friar Court ya kasri la St. James mjini London saa tano saa za huko, muda unaoambatana na mbwembwe za wapiga tarumbeta, milio ya bunduki zinazofyetuliwa kwa heshima katika bustani ya Hyde na katika Jumba refu maarufu la London Tower.

Licha ya kwamba sio sehemu ya shughuli hiyo rasmi ya kutangazwa mfalme, maneno "Malkia amefariki, Mflame aishi Maisha marefu" mara nyingi hutamkwa baada ya hapo.

Siku ya Ijumaa, Charles alikutana na umati wa watu waliopiga kelele "God save the King!" yaani Mungu mlinde Mfalme wakati akisalimiana na umati uliokuwepo nje ya kasri la Buckingham.

Baada yah apo alitoa hotuba kwenye televisheni akieleza matumaini kwamba Mwanawe William kama Mwanamfalme mpya wa Wales na mkewe Catherine - "wataendelea kuwatia watu moyo na kuongoza mdahalo wa kitaifa".

Matukio ya leo:

  • Baraza la kumtangaza Mfalme, hafla rasmi kumtangaza Charles kama mfalme litafanyinka 10:00 BST
  • Kuanzia saa tano, saa za London, Bendera zitapepea kikamilifu na kufuatwa kwa milio ya bunduki zilizofyetuliwa kwa heshima Matangazo ya ziada yatatolewa kutoka roshani ya kasri la St James na mjini London
  • Maafisa wakuu serikali watakula kiapo cha Mfalme Charles III katika bunge la wawakilishi
  • Ameelezea "mapenzi yake kwa Harry na Meghan" na kupongeza mkewe Malkia Camilla kwa " uwajibika imara kwa majukumu ".

Mfalme amekiri kuwa Maisha yake yamebadilika sasa, akieleza kuwa hatoweza kutoa "muda zaidi na nguvu" kwa wakfu mbali mbali na masuala ambayo alitoa usaidizi kwa miongo kadhaa kama mrithi wa kiti cha enzi.

Nini hufanyika katika baraza la kumtangaza Mfalme?

  • Kihistoria, hafla hii huhudhuriwa na baraza la washauri wa ufalme ambalo limekuwepo tangu enzi la wafalme wa Norman. Wakati wanabaraza wakiwa ni 700, wengi wakiwa ni wanasiasa wa zamani na wa sasa, ni wanabaraza 200 pekee watakaokusanyika.
  • Awali wanakusanyika katika kasri la St James pasi mfalme kuwepo. Mbunge wa chama cha Conservative Penny Mordaunt, aliyeteuliwa kuwa rais wa baraza na Waziri mkuu Liz Truss, atatangaza kifo cha Malkia
  • Karani wa baraza hilo atasoma tangazo rasmi la Mfalme akijumuisha jina la Charles kwamba ndiye anayepokea wadhifa wa Mfalme – ambaye tunayemfahamu kama Charles III.
  • Tangazo hilo linatiwa Saini na kundi akiwemo mkewe mfalme, Mwanamfalme wa Wales na askofu mkuu wa Canterbury, kiongozi mkuu bungeni, askofu mkuu wa York na Waziri mkuu.
  • Rais wa baraza ataomba ukimya na kisha asome ratiba ya shughuli zilizosalia, akishughulikia matangazo ya umma na amri za ufeytuaji bunduki kutoa heshima katika bustani ya Hyde na jumba refu maarufu la London Tower.
  • Mfalme anaingia katika awamu ya pili ya baraza hilo linalohudhuriwa na wanabaraza wakuu na kutoa tangazo binafsi kuhusu kifo cha Malkia
  • Anakula kiapo kulihifadhi kanisa la Uskotchi na kusaini nyaraka mbili ili kunakili, huku Malkia mkewe na mwanamfalme wa Wales wakishuhudia. Wanabaraza wakuu watasaini tangazo hilo huku wakiondoka.