Malkia Elizabeth: Mapenzi yake katika mbio za farasi

ggg

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Malkia, akiwa katika picha ya pamoja na meneja wake wa mbio za farasi John Warren, alishinda zaidi ya £150,000 kama pesa za zawadi kwa ushindi wa Estimate Gold Cup.

Jambo la kwanza unatakalo litambua unapofika kwenye makazi ya mapumziko ya Malkia ni sanamu ya ukubwa karibu sawa na farasi wake wa mashindano.

Sanamu huyo huko Sandringham ni ushuhuda wa mapenzi yake makubwa na ya kudumu katika mbio za farasi, mchezo ambao ulitoa muonekano nadra wa mtu tofauti na taji la Umalkia.

Wakati Estimate (Farasi) iliposhinda Kombe la Dhahabu katika mashindano ya Royal Ascot mnamo 2013, ilikuwa mara ya kwanza kwa kiongozi wa kifalme anayetawala kumiliki mshindi katika kipindi cha miaka 207. Alinaswa kwenye kamera akitabasamu kwa furaha kutoka kwa chemba ya Kifalme pamoja na meneja wake wa mbio John Warren.

"Zinapomalizika na matokeo kama hayo, hakika ni mwisho wa safari ya kushangaza," alisema.

Ushindi wa Farasi Estimate ulikuwa kati ya jumla ya ushindi wa zaidi ya 1,800 katika mashindano ya mbio za zambarau, dhahabu na nyekundu. Na Malkia alitambuliwa kwa mchango wake katika mbio za farasi kama mmiliki na mfugaji kwa kuingizwa katika Orodha ya heshima ya Mabingwa wa Uingereza mnamo 2021.

Mashindano ya mbio za farasi yalimpa malkia kujiweka pembeni kidogo na mambo ya busara zaidi ya maswala ya kimataifa na ya ndani.

"Alikuwa akiniambia: 'Inapendeza kufika sehemu ambayo haina harufu ya rangi mpya'," mkufunzi Richard Hannon alisema. Nakala ya gazeti la Racing Post iliwekwa kila siku katika mawasiliano yake ya kila siku.

ggg
Maelezo ya picha, Sanamu ya inayokadiriwa kuwa sawa na farasi wa mashindano ikiwa huko Sandringham

Farasi walikuwa ndani ya maisha yake tangu utotoni. Malkia alijifunza kupanda farasi wa Shetland inayeitwa Peggy, zawadi ya nne ya siku ya kuzaliwa kutoka kwa babu yake George V.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mapenzi yake katika mbio yaliongezeka wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alipoandamana na baba yake kuona farasi wa kifalme wakifanya mazoezi huko Wiltshire.

"Niliweza kuwapiga-piga kwenye mazizi baadaye," alikumbuka baadaye.

Malkia alionekana hadharani kwa kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa mbio za farasi wiki mbili baada ya kumalizika kwa vita huko Ulaya Mei 1945, aliongozana na wazazi wake kwa mara ya kwanza hadi Ascot.

Mkutano wa Royal Ascot ulikuwa moja ya hafla zake za kijamii alizopenda na alifurahia kupata jumla ya ushindi mara 24.

Kila mwaka, Malkia alikuwa akifika kwa maandamano kutoka kasri la Windsor na washika dau walikuwa wakiweka dau kuhusu kofia ya rangi gani ambayo angevaa ambapo bluu ilikuwa ikichaguliwa kwa wingi.

Ilikuwa kutoka kwa baba yake, Mfalme George VI, kwamba Malkia Elizabeth II arithi farasi kutoka Royal Stud, kituo cha kuzaliana farasi wa mbio huko Sandringham ambacho kimetoa washindi wake wengi.

Ushindi wake wa kwanza ulikuja na farasi aliyeitwa Monaveen baada ya kuruka huko Fontwell Park mnamo 1949, na alikuwa bingwa mara mbili mnamo 1954 na 1957.

"Alitambua farasi wake kwa kuwaona, alivutiwa na ukuaji wao wa kiakili na kimwili na siku zote alizungumza kwa kina na mfanyakazi anayemtunza kila farasi," alisema mtangazaji Clare Balding, ambaye babu, baba na kaka yake wote wamewafundisha farasi wa Malkia.

"Mfano mmoja mdogo makini wa ndani ulikuwa Malkia hakuwahi kujipulizia manukato alipotembelea yadi kuona farasi wake kwani inaweza kusisimua homoni ya testosterone kwa farasi wadogo," alisema.

"Malkia alikuwa mfuasi mzuri wa Monty Roberts aliyekuwa na uwezo wa kumsikiliza farasi na kumuelewa na alitumia mbinu nyingi za Monty kwa Farasi wachanga na wale wa mwaka kwa mfano, kuwaongoza juu ya karatasi ya bluu ya plastiki ili wasiogope kutembea kwenye maji.

"Matokeo yalikuwa kwamba walikuwa wasikivu zaidi na wenye tabia nzuri zaidi walipofika kwenye viwanja vyao mbalimbali vya mashindano."

Alikuwa akitoa jina kwa farasi, mara nyingi lenye ujumbe wa wazi kama vile Wajibu, Katiba na Busara.

ggg
Maelezo ya picha, Malkia aliendelea kupanda farasi hadi miaka ya 90

Mkufunzi Sir Michael Stoute, ambaye alisimamia washindi zaidi ya 100 wa kifalme ikiwa ni pamoja na Estimate, alisema alikuwa na furaha kufanya kazi hiyo.

"Niligundua kuwa kutoa mafunzo kwa Malkia haikuwa kazi sana, kwa sababu ya ufahamu wake, ujuzi wake wa kina na kiu yake ya zaidi," alisema.

"Siku zote alikuwa akifikiria mbele nitafanya nini na mnyama huyu, nitamfuga, nimzalishe na yupi, tabia, kasi, stamina. Alivutiwa na wazo zima."

Mmoja wa wapanda farasi wake wake aliowapenda sana alikuwa Frankie Dettori, na mara nyingi wawili hawa walifanya mzaha pamoja baada ya ushindi wa mbio kubwa, kama Dettori alivyokumbuka baada ya ushindi wa King George VI na Malkia Elizabeth Stakes huko Ascot.

"'Huyo ni Mfalme wangu wa nne George,' nilisema. Malkia alinitazama na kuinua nyusi: 'Lester (Piggott) alishinda saba.' Niliambiwa hivyo," alisema.

ggg
Maelezo ya picha, Frankie Dettori alikuwa mmoja wa wapanda farasi wa Malkia

Akiwa mmiliki, Malkia alishinda mbio nne kati ya tano za British Classic.

Farasi Dunfermline alishinda mashindano ya Oaks mwaka 1977 siku tatu kabla ya sherehe zake za maadhimisho ya miaka 25 ya ndoa na pia alishinda St Leger baada ya mafanikio ya awali na Carrozza (Oaks 1957), Pall Mall (2,000 Guineas 1958) na Highclere (1,000 Guineas 1974).

Ushindi wa Estimate huko Ascot miezi 12 baadaye ulizaa zaidi ya £150,000 kama pesa za zawadi na Malkia akawa amepata mamilioni kwa miaka, ingawa mengi ya hayo yalipunguzwa na ada za mafunzo na gharama zingine.

Warren alisema farasi walikuwa "kikimbilio kubwa" kutokana na majukumu mengine na uungaji mkono wake umekuwa msaada mkubwa kwa mbio za Uingereza.

"Nina hakika kama Malkia hasingekuzwa kuwa Malkia alikuwa na wito kwa farasi. Ilikuwa tu katika DNA yake," alisema.