Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, ni nani washindi na walioshindwa Ligi Kuu ya England barani Afrika?
Pazia limeshushwa katika kampeni za Ligi Kuu ya 2023-24, huku Manchester City ikiweka historia kwa kunyakua taji la nne mfululizo.
Miezi 12 iliyopita Riyad Mahrez alikuwa sehemu ya kusherehekea kombe la The Blues lakini baada ya winga huyo wa Algeria kuhamia Saudi Arabia mabingwa hao hawana tena Mwafrika yeyote katika kikosi chao cha kwanza
Hapa BBC Sport Africa inachagua wachezaji wachache kutoka barani kote ambao wamevutia macho, kwa bora au ubaya, katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.
Baadhi wanaweza kuvutia soko la uhamisho, wakati wengine watakuwa na wasimamizi wapya wa kufanya kazi chini yao msimu mpya utakapoanza Agosti.
Washindi: Yoane Wissa (Brentford)
Katika msimu wa kusikitisha kwa The Bees , mabao 12 ya Wissa yalikuwa muhimu sana katika kuepusha kushushwa daraja.
Kufikia kiwango chake bora zaidi England, aliongoza safu ya Brentford kwa ustadi kwa muda mrefu bila Ivan Toney aliyesimamishwa na kumjeruhi Bryan Mbeumo.
Fowadi huyo alifanikiwa yote licha ya kukosa mwezi mmoja wa msimu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), ambapo aliisaidia DR Congo kutinga nusu fainali kabla ya kushindwa na mabingwa na wenyeji Ivory Coast.
Si mchezaji wa sehemu ndogo tena, itapendeza kuona ni kiasi gani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuendeleza msimu ujao - hasa Toney akitarajiwa kuondoka.
Nicolas Jackson (Chelsea)
Mshambulizi huyo wa Senegal alikuwa na msimu wa kwanza akiwa na Chelsea, ambao bado wana kazi kubwa licha ya kutumia $1.23bn (£1bn) katika uhamisho tangu kununuliwa na Todd Boehly.
Jackson alifunga mara mbili pekee katika mechi zake saba za kwanza za ligi - huku akiendelea kufungiwa - kabla ya kufunga hmabao matatu katika ushindi wa fujo dhidi ya wachezaji tisa Tottenham.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alijitahidi kufanya vyema kati ya Novemba na Machi lakini kiwango chake mwishoni mwa msimu, alifunga mabao manne huku Chelsea ikishinda mechi zao tano za mwisho, na kuashiria mustakabali mzuri kwa Mwafrika huyo wa Magharibi.
Hata hivyo, iwapo Mauricio Pochettino atasalia dimbani au The Blues kuamua kusajili washambuliaji zaidi kunaweza kuathiri muda wake wa kucheza Stamford Bridge.
Mohammed Kudus (West Ham)
Mghana huyo ameharibu sifa yake ya kuwa tishio baada ya uhamisho wa pesa nyingi kutoka Ajax.
Baada ya kipindi cha utulivu Kudus alifikisha kilele cha ubora wa juu mnamo Desemba mtindo wake wa kipekee wa kusherehekea kufunga bao umemfanya kuwa kwenye ukumbi wa matangazo ya uwanja na kuwa jambo la kawaida kwa mashabiki
Black Stars ilivumilia kuondolewa tena mapema Afcon lakini Kudus alimaliza akiwa na mabao 14 na pasi za mabao sita katika mashindano yote kwa The Hammers huku klabu hiyo ikikosa kucheza soka la Ulaya msimu ujao.
Julen Lopetegui anatazamiwa kuchukua nafasi ya David Moyes katika klabu hiyo ya London mashariki, na bila shaka Mhispania huyo atakuwa na nia ya kusalia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 iwapo klabu kubwa zitamwita mara tu dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.
Antoine Semenyo (Bournemouth)
Matokeo ya Bournemouth chini ya bosi mpya Andoni Iraola yalishangaza wengi, na umbo la fowadi wa Ghana Semenyo lilieleza mabadiliko hayo kikamilifu.
Haraka na bila kuchoka, aliwapa mabeki wakati mgumu na kuwa nyota kwa kuanza katika kila mechi
Ongeza mabao manane na inakuwa wazi Bournemouth ilifanya biashara yenye tija ilipotumia £10m ($12.7m) kumleta kutoka Bristol City Januari 2023.
Uimara wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia ulithibitishwa na ukweli kwamba hakukosa mechi, alishiriki katika mechi 33 za Ligi Kuu ya England na 10 za kimataifa kwa Black Stars.
Sifa za heshima ziende kwa...
Baada ya muda wa mkopo nchini Ubelgiji msimu uliopita, Simon Adingra alifunga bao lake la kwanza kwa Brighton na kumalizia na mabao sita ya ligi.
Lakini utukufu wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ulikuja na Ivory Coast kwenye Afcon, ambapo alifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama kwenye robo fainali dhidi ya Mali na kisha kuweka mabao yote mawili kwenye fainali huku The Elephants wakinyakua taji lao la tatu la bara.
Mwanzoni mwa Aprili, Everton walikuwa wameshikilia rekodi ya klabu katika mechi 13 za Ligi Kuu ya England bila kushindwa na kuchupa kushuka daraja.
Sogeza mbele shujaa ambaye haonekani kama Idrissa Gana Gueye, ambaye alifunga mara tatu katika mechi sita za mwisho, akigeuza saa na kuonyesha mchezo mzuri uliompa kiungo huyo mkongwe wa Senegal kandarasi mpya.
Wakati huo huo, hii ilikuwa kampeni ya Rayan Ait-Nouri alikomaa na kujigeuza kuwa chaguo la kwanza kwa Wolves na Algeria.
Tishio kubwa mbeleni, beki huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 22 amehusishwa na uhamisho wa kwenda timu tatu zilizopigania taji msimu huu
Waliopoteza: Mohamed Salah (Liverpool)
Kwa mwanamume ambaye alikuwa Mwafrika aliyefunga mabao mengi zaidi msimu huu akiwa na mabao 18 ya Ligi Kuu, inaweza kuonekana ajabu kuona jina la Salah likiwa miongoni mwa waliopoteza.
Kufumania nyavu mara moja tu katika mechi saba za mwisho za ligi kulimfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kumaliza na idadi ndogo zaidi ya mabao yake tangu ajiunge na Liverpool mwaka 2017.
Msimu wa Salah ulikatizwa na jeraha la msuli wa paja akiwa Misri kwenye Kombe la Mataifa, na pia alikosa ushindi wa fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Chelsea.
Kisha ikafuata kufuzu kwa Liverpool kwa Ligi ya Europa katika robo-fainali na makabiliano ya hadharani na kocha anayeondoka Jurgen Klopp huku changamoto ya kuwania taji la Reds ikififia.
Kandanda ya Ligi ya Mabingwa ina uhakika wakati Arne Slot akielekea Anfield bado, huku wachumba nchini Saudi Arabia wakijitokeza, je Salah atatafuta mwanzo mpya?
Yves Bissouma (Tottenham)
Tottenham walianza msimu huu chini ya bosi mpya Ange Postecoglu wakiwa katika kiwango kizuri na walikuwa kileleni mwa jedwali mwishoni mwa Oktoba.
Kisha ukafuata msururu wa mechi tano bila ushindi kabla ya Bissouma kusalia nje mechi tatu za mwisho za 2023 kwa kufungiwa baada ya kupata kadi nyekundu ya pili msimu huu.
Ugonjwa wa malaria uliathiri kiwango cha kiungo huyo kwenye Afcon na Spurs wakakosa kucheza Ligi ya Mabingwa baada ya kushindwa mara nne mfululizo mnamo Aprili na Mei.
Bissouma hakuwepo katika mechi mbili za mwisho za msimu huu kutokana na jeraha la goti, ambalo linaweza pia kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoshiriki mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 nchini Mali mwezi ujao.
Sofyan Amrabat (Manchester United)
Kama mmoja wa watu muhimu katika kampeini ya kihistoria ya Morocco hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia la 2022, Amrabat alitarajiwa kuongeza safu ya kiungo ya United baada ya kujiunga kwa mkopo kutoka Fiorentina.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alianza mechi 10 pekee za ligi huku Mashetani Wekundu wakiandika mwisho wao mbaya zaidi (wa 8) tangu ligi kuu ya Uingereza ilipobadilishwa jina mwaka 1992.
Kikosi cha Erik ten Hag pia kiliangukia nje ya Uropa mapema na Amrabat akatolewa kwa kadi nyekundu huku timu ya Morocco iliyokuwa ikishabikiwa sana na Afrika Kusini katika hatua ya 16 bora kwenye Afcon.
Matumaini ya mwisho ya United katika soka la bara msimu ujao ni kuwashinda wapinzani wao City katika fainali ya Kombe la FA - lakini iwapo watalipa euro milioni 20 ($21.7m, £17.1m) kufanya mkataba wa Amrabat kudumu ni suala jingine.
Issa Kabore (Luton Town)
Kwa mkopo kutoka kwa Manchester City, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alishindwa kupata matokeo ambayo wengi walitarajia angeweza - ingawa ni sawa kusema kwamba kampeni yake ilikwama katikati ya Afcon na jeraha la msuli wa paja liliongezeka muda mfupi baada ya kurudi.
Kabore alianza mechi 21, mara nyingi akiwa beki wa pembeni wa kulia, na kutoa pasi mbili za mabao huku Hatters wakishushwa daraja.
Sasa atarejea kwenye timu ya washindi wa taji, lakini mustakabali wa muda mrefu wa raia huyo wa Burkina Faso huko Etihad upo mashakani.
Maneno yasiyo ya heshima yaende kwa.....
Manchester United ililipa karibu $60m (£47.2m) kumsajili Andre Onana kutoka Inter Milan Julai mwaka jana na ni salama kusema uamuzi bado haujatolewa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alifanya vyemakukosa kufungwa mabao mara tisa nyuma ya safu ya ulinzi inayobadilika kila mara - nambari moja tu nyuma ya mpinzani wa Manchester City Ederson - lakini pia kulikuwa na msururu wa makosa ya hali ya juu.
Wakati huohuo, kuwasili tu siku ya mechi ya kwanza ya Cameroon Afcon ilikuwa taswira mbaya na alianza mchezo mmoja tu kati ya nne za taifa lake katika mashindano hayo.
Ibrahim Sangare wa Ivory Coast alikuwa na Afcon bora zaidi, aliyoshiriki katika mechi sita kati ya saba, lakini athari yake huko Nottingham Forest kufuatia kuripotiwa kununuliwa kwa $38m (£30m) kutoka PSV Eindhoven ilikuwa chini ya ilivyotarajiwa kwa usajili uliovunja rekodi ya klabu.
Kiungo huyo wa kati alicheza mechi 13 katika timu ambayo ilikuwa na matatizo, bila kuchangia mabao na bila kutoa pasi za mabao.
Sheffield United ilisajili wachezaji watatu wa Kiafrika kabla ya msimu huu lakini, kama klabu yenyewe, wote walitatizika vibaya.
Beki wa pembeni wa Algeria, Yasser Larouci aliingia kwa mkopo kutoka Troyes na alifanikiwa kuanza ligi mara sita tu, kumaanisha lazima iwe na shaka kwamba Blades sasa wataanzisha kipengele cha kufanya uhamisho wake kuwa wa kudumu kufuatia kushushwa daraja.
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah