Je, mlo wako unaathiri uwezo wako wa kupata ujauzito?

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, vyakula sahihi vinaweza kuboresha uwezekano wako wa kupata mtoto? Ukweli ndio huu.

Ukitembelea kurasa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii inayojihusisha na masuala ya afya ya uzazi moja ya mada kuu inayojadiliwa kwa kina mtandaoni, ni aina gani ya chakula inayofaa kutumika ili kusaidia kuongeza uwezo wa kubeba ujazito kwa haraka.

Ukiachilia mbali matumzi makubwa ya virutubisho vinavyosaidia kubeba ujauzito kuna aina nyingi ya vyakula vinavyoweza kusaidia kwenye afya ya uzazi na ujauzito.

Ukiachilia mbali maelezo mengi ya afya ya uzazi na sera za wafanyabiashara kuhusu suala la uzazi, kuna ushahidi gani halisi wa kutumia vyakula fulani ili kuimarisha uzazi kwa wanaume na wanawake pamoja na ukuaji mzuri wa mtoto aliye tumboni ?

Jambo la kwanza, linapokuja suala la kusaidia ujauzito salama na ukuaji wa mtoto aliye tumboni, virutubisho fulani vinaweza kusaidia kuleta mabadiliko kama vile vitamini ya Folic acid. Vitamini hivi vikitumika kabla na wakati wa ujauzito, imeoneshwa kusaidia kuzuia tatizo la anencephaly, inayoathiri ubongo wa mtoto na bifida tatizo linaloathiri mgongo wa mtoto.

Kwa sababu matatizo haya huwa yanaanza mapema kipindi cha ujauzito mara nyingi hata kabla ya mwanamke kujua kwamba ana ujauzito, Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Marekani vinapendekeza kwamba wanawake wote walio katika umri wa kuzaa wanywe mikrogramu 400 (mcg) za folic Acid kila siku.

Kuimarisha vyakula vikuu kama vile nafaka zenye asidi ya foliki kunaweza kutoa ulinzi wenye nguvu zaidi, kwa sababu mimba nyingi hazijapangwa.

Inakadiriwa kuwa, mnamo 2019, mipango madhubuti ya matumizi ya Folic Acid kwa asilimia 22 ili kuweza kuzuia matatizo ya ubongo na uti wa mgongo kwa watoto wadogo kote ulimwenguni.

Folic Acid inaweza kuwa na faida ya nyingi pale mwanamke anayetaka kupata mimba akitumia.

Vipi kuhusu vyakula vingine na virutubisho? Kuna kitu kama "lishe ya uzazi" ambayo itasaidia kwenye safari ya kupata mimba?

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Utafiti wa wanandoa wanaopitia IVF( Tiba ya urutubishaji watoto) uligundua kuwa ulaji wa nyama kwa wanaume, na haswa aina ya nyama wanayokula, huathiri urutubishaji

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ili kujibu swali hilo, inasaidia kuondoa hali ya kutopata ujauzito utasa. Nchini Marekani, baada ya mwaka mmoja wa kufanya tendo la ndoa bila kinga, asilimia 15 ya wanandoa hawawezi kubeba mimba.

Kuna sababu nyingi za hali hii kutokea . Kwa upande wa wanawake, kiungo cha uzazi kinaweza kushindwa kuzalisha mayai yenye afya, au yai haliwezi kusonga kutoka kwenye kiungo cha uzazi kwenda kwenye tumbo, kwa mfano, kutokana na kuziba kwa mirija ya uzazi yaani fallopian.

Hata kama yai litafanya safari hiyo kwa mafanikio, basi huenda lisishikane na utando wa tumbo la uzazi, au lisiishi mara linaposhika.

Kwa upande wa mwanaume, ubora wa mbegu za kiume ni muhimu kwa uzazi.

Hii ni pamoja na uwezo wao wa kutembea kwa ufanisi, umbo na ukubwa wao,

Sababu mbalimbali zinaweza kutishia ubora wa mbegu za kiume, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kimazingira kama vile uchafuzi wa mazingira . Hata baada ya vipimo, sababu ya kutobeba ujauzito haiwezi kuwa wazi kila wakati: karibu asilimia 15 hali ya kutobeba mimba hubakia bila kuelezewa.

Ingawa hakuna chakula cha mtu binafsi au kirutubisho kitakuwa suluhu ya haraka kwa mojawapo ya masuala haya yanayoweza kutokea, wataalamu wanasema lishe inaweza kuwa na jukumu la manufaa katika mchakato wote wa kujaribu kupata mimba na zaidi.

Kwa wazi zaidi, lishe bora ni muhimu. Matokeo ya utapiamlo yanaweza kuwa mabaya kwa afya ya kabla ya kujifungua.

Bila shaka matokeo yanayojulikana zaidi katika eneo hili yanatokana na utafiti wa watoto waliotungwa wakati wa kile kinachoitwa "Kipindi cha baridi cha njaa cha Uholanzi" cha 1944; njaa ya miezi minane ambayo ilitokea wakati Wanazi walipoacha kutoa chakula nchini Uholanzi mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia.

Akina mama walikuwa wakiishi kwa milo yenye mafuto gramu 400 tu kwa siku, sehemu ya ulaji unaohitajika kwa ujauzito wenye afya. Watoto waliotungwa mimba wakati huo walikabiliwa na aina mbalimbali za madhara ya kiafya, ikiwa ni pamoja na kuwa wafupi kwa kimo na wembamba kuliko waliozaliwa kabla au baada yao, na kuwa na vichwa vidogo. Wakiwa watu wazima, walikuwa na viwango vya juu vya unene wa kupindukia, kisukari na wengine kufa wakiwa wachanga zaidi.

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa wale ambao wanaweza kupata chakula cha kutosha, bado ni muhimu kupata mchanganyiko sahihi wa virutubisho. Ingawa mijadala kuhusu vyakula vyenye manufaa mara nyingi huzingatia uzazi wa mwanamke, kumekuwa na ufahamu unaokua wa jinsi chakula kinaweza pia kuathiri uzazi wa kiume.

Utafiti wa mwaka 2015 wa wanandoa wanaopitia IVF uligundua kuwa ulaji wa nyama kwa wanaume, na haswa aina ya nyama waliyokula, iliathiri urutubshaji,. Kula kuku zaidi kulikuwa na matokeo mazuri katika viwango vya kutunga mimba, ambapo kula nyama iliyochakatwa (kama vile nyama ya nguruwe na soseji) kulikuwa na athari mbaya. Wanaume ambao walikula nyama iliyosindikwa kidogo zaidi, wastani wa chini ya moja nukta tano kwa wiki, walikuwa na nafasi ya hadi asilimia 82% ya kuwapa ujauzito wenzi wao - wakati wanaume ambao walikula nyama iliyosindikwa zaidi, kwa wastani wa 4.3 kwa wiki, walikuwa na hadi asilimia 54 tu ya uwezo wa kuwapa ujauzito wenzi wao.

Hata baada ya kupata mimba, lishe ya baba inaweza kuathiri ukuaji wam toto tumbo japo sio moja kwa moja.

Utafiti ulioongozwa na watafiti katika Chuo Kikuu cha Queensland nchini Australia umeonyesha kwamba kile ambacho akina baba hula kina athari ya kudumu kwa afya ya wakati ujao ya watoto wao ambao hawajazaliwa. Watafiti hao walichambua data ya lishe kutoka kwa karibu wanandoa 200 wanaopokea huduma ya ujauzito katika hospitali kubwa zaidi ya uzazi ya Australia, Hospitali ya Mama wa Mater huko Brisbane. Utafiti huo uligundua kuwa ulaji wa chakula cha wanaume huathiri sana ule wa wanawake, na hivyo iliathiri mtoto anayekua. Uchunguzi mwingine unaonyesha kwamba uzito wa baba unaweza kuwa na athari kati ya vizazi, kuathiri uzito wa mtoto.

"Afya ya wanaume na lishe kwa ajili ya uzazi hazizingatiwi, lakini ni muhimu sana," anasema Shelley Wilkinson, mtaalamu wa lishe ambaye alikuwa mmoja wa waandishi wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Queensland na sasa anafanya kazi katika kliniki ya uzazi Lifestyle, kliniki ya kibinafsi nchini Australia ambayo inashughuliki masuala ya uzazi. "Kwa kweli inaweza kuathiri afya ya wajukuu wao."

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Wilkinson pia anaangazia umuhimu wa kushughulikia mabadiliko yoyote kama wanandoa. "Ikiwa mtu mmoja anakutana na miongozo ya lishe, mtu mwingine ana uwezekano mkubwa wa kuwa vile vile," anasema. "Tunapaswa kuzingatia kusaidia wanawake na wanaume kufanya mabadiliko yenye afya. Vinginevyo, tunapoteza nusu ya vita."

Badiliko moja la manufaa linaweza kuwa kuongeza kiwango cha mafuta katika mlo wa wanandoa mradi tu ni aina sahihi ya mafuta. Mafuta yenye afya hupatikana katika karanga, , parachichi na mafuta ya mizeituni. Hata hivyo, asidi ya mafuta ya trans ambayo inaweza kutoka kwa vyanzo vya asili au viwanda, na kwa mfano hupatikana katika margarine, donuts, vyakula vya kukaanga na vyakula vingine vilivyotengenezwa - vinahusishwa na hatari kubwa ya utasa.

Lishe yenye wingi wa mimea pia inaweza kuwa na manufaa. Watafiti katika Shule ya Harvard ya Afya ya Umma walitathmini mlo wa kundi la wanawake 18,555 zaidi ya miaka minane, walipojaribu kupata ujauzito au kupata mimba. Kutumia protini inayotokana na mimea kama vile kunde, badala ya protini zinazotokana na nyama kama vile nyama nyekundu, kulihusishwa na hatari ya chini ya zaidi ya asilimia 50 ya hali ya kutopata ujauzito.

Tunahitaji kuwasaidia wanawake na wanaume kufanya mabadiliko ya kiafya. Vinginevyo, tunapoteza nusu ya vita - Shelley Wilkinson

Waandishi wa hakiki ya mwaka 2021 ya utafiti kuhusu uhusiano unaowezekana kati ya lishe na uzazi kwa wanawake walihitimisha kuwa, ingawa mapendekezo yao yalilenga wanawake, "mifumo ya lishe na lishe bila shaka ni muhimu kwa uzazi pande zote mbili , mwanaume na mwanamke.

Watafiti walitoa dondoo za kina za athari za virutubishi vya mtu binafsi na vyakula vilivyomo. Pia walisisitiza umuhimu wa kuhusisha mtaalamu wa lishe katika huduma ya wanandoa wanaopanga kupata ujauzito. Kwa ujumla, walipendekeza kuwa vyakula kama vile mboga, matunda, tambi na mkate wa nafaka nzima ni vyanzo vya mafuta yenye afya kama vile samaki wenye mafuta; na kunde, mayai na nyama konda kwa ajili ya protini. Pia walionyesha jukumu muhimu la virutubisho fulani ambavyo wakati mwingine vinaweza kupuuzwa: hizi ni pamoja na iodini, ambayo husaidia maendeleo sahihi ya mtoto alie tumboni na mama mjazito.

yyy

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa pombe, ushauri ni wazi na thabiti katika utafiti wote. CDC inasema: "hakuna kiwango salama kinachojulikana cha matumizi ya pombe wakati wa ujauzito au wakati wa kujaribu kupata mimba." Hii inatumika kwa aina zote za pombe, pamoja na divai zote na bia. Ushauri ni kuepuka kabisa.

Ikiwa una wasiwasi wowote au maswali kuhusu mlo wako na jinsi unavyoweza kuathiri uzazi wako, hatua bora ni kushauriana na mtoa huduma wako wa afya. Na ingawa baadhi ya vyakula vinaonekana kuwa na nafasi nzuri katika uzazi, ni muhimu kutozidisha nguvu zao.

Wilkinson anasema kuwa watu walio na matatizo ya uzazi mara nyingi wanatafuta chakula kimoja cha kukuza uzazi lakini ni bora kulenga mtindo wa ulaji wa afya kwa ujumla. "Katika vyumba vya mazungumzo ya uzazi, kuna mazungumzo mengi kuhusu nanasi kuwa aina fulani ya chakula cha kichawi cha rutuba ikiwa unajaribu kupata mimba. Hata hivyo, hakuna chakula kimoja au kirutubisho kinachofanya kazi hivyo."