Wazazi wanaowalea watoto wao bila utambulisho wa jinsia

Wakati Gabriella Martenson alipojiandaa kwa ajili ya kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza, alichukua uamuzi. Aliamua kuwa hatawahi kumwambia mtoto wake iwapo alizaliwa mvulana au msichana na ataepuka sana kujadiliana naye kuhusu jinsia yake ya kuzaliwa na watu nje ya familia yake na kundi la marafiki zake.

“Ninataka awe anavyotaka kuwa. Sitaki kuamua hilo kwa niaba yake,” anasema Martenson, ambaye alikuwa na umri wa miaka 30 na kuishi katika nyumba yake katika mji wa kwa owa Stockholm, alipopata mtoto wake wa kwanza.

“[Ni ] kwamba tu sitaki kuamuamulia awe mtu wa aina gani wakati atakapokuwa mtu mzima na ni nini atakachotaka kufanya, au ni nani atakayeamua kumpenda au kuishi naye.”

Kama mtoto binafsi, Martenson alilelewa katika kanuni zenye mtizamo fulani kuhusu jinsia , kama vile kupewa vitu vyenye rangi ya waridi kama vile magauni avae.

Lakini alipofikisha miaka karibu ishirini, alisema “niligundua uanaharakati wa wanawake” na akaanza kuhoji kuhusu kanuni za jinsia. Kwahiyo alivyokuwa mama, alimua kununua nguo kwa mtoto wake za aina mbali mbali na zawadi, kuanzia pamoja na wanasesere (midoli), na kuwapatia uhuru wa kuchagua wanachotaka kutumia kila siku.

Alitumai aina yake ya malezi ya mzazi yatamsaidia mtoto wake kuhisi zaidi kuwa na urahisi wa kugundua mambo wanayoyapenda zaidi na kujifunza, kuliko kuwaongoza kufanya shughuli zinazobagua jinsia.

Waandishi wa malezi ya wazazi, wanasaikolojia na waalimu wa watoto wa shule za awali wanasema wamegundua kuwa mtindo huu wa malezi umeanza kushamiri katika muongo uliopita, hususani katika mataifa ya Ulaya Kaskazini na Marekani.

Kuongezeka kwa malezi yasiyoegemea jinsia

Mwandishi wa Berlin- kuhusu malezi na mhadhiri Ravna Marin Nathanael Siever anasema kuamua kutomuita mtoto msichana au mvulana ni jambo ambalo lilianza kupata umaarufu katika miaka 1980, hasa katika jamii za watu ambao hawamini kuwa wako katika jinsia yoyote ile(queer). Hii iliambatana na kile wanachokielezea kama “wimbi la pili la utetezi wa jinsia ya kike”, huku wanawake wengi wakipinga kuitwa kama wasaidizi wa nyumbani au katika kazi za aina fulani.

 Malazi ya wazazi ya usawa katika jinsia, yalijitokeza sio kuweka usawa wa jinsia za watoto, “bali kuwaruhusu kugundua utambulisho wao wao wenyewe, kuliko kuambiwa utambulisho wao na watu wengine”, anasema Siever.

‘Wanaweza kuishi maisha wanayohisi ni bora kwao’

Malezi ya usawa wa kijinsia yanatofautiana – na namna yanavyotekelezwa na na wazazi mara nyingi huwa ni ya kibinafsi, kulingana na mtizamo wa jamii zao na uzoefu.

Miongoni mwa familia, moja ya chaguo la nchi zinazozungumza Kiingereza ni kwa wazazi kuwaelezea watoto wao kwa kutumia viwakilishi wenyewe/wao (they/them). Neno ‘theyby’ – mchanganyiko wa maneno ‘they’ na baby’ – yamejitokeza katika kuelezea watoto hawa. Baadhi ya wazazi wanapendelea kutumia mchanganyiko wa viwakilishi vya jinsia ‘he’ na ‘she’ badala yake.

Wanandoa kama vile, Martinson, huwanunulia watoto wao nguo “ za kike na za kiume”, na kujaribu kuwapatia chaguo pana zaidi la umiliki na burudani.

“Tunahakikisha kuwa wanasoma vitabu au kutazama filamu ambazo zinawakilisha aina fulani ya jinsia zote, na ambazo hazielezei zaidi kanuni nyingi zenye ubaguzi wa jinsia fulani ,” anasema.

Athari zisizojulika

Kwasababu malezi ya kutozingatia jinsia yoyote badio ni ya hivi karibuni zaidi na tafiti kuyahusu bado ni chache, watafiti bado hawajui athari zake za muda mrefu ni zipi,ikiwa ni pamoja na jinsi yanavyowaathiri watoto na jamii kwa ujumla.

Wanaounga mkono malezi haya wanadai kuwa yanaleta mabadiliko , walau kwa mu binafsi.

Kwa pamoja Tschannen na Martinson wako wazi kwamba malezi ya kutozingatia jinsia hayakomi wakati mtoto anapochagua jinsia anayotaka kujitambulisha nayo. Kwa mfano, wanajaribu kuepuka kutumia lugha inayobagua jinsia nyingine nyumbani

 “Wakati ninapozungumza kuhusu watoto. Kama ni mtu fulani tunayemfahamu vyema , ninaweza kusema ‘she‘ au ‘her’. Lakini kama ni mtoto katika eneo lao la kucheza, ninawaita tu ‘’rafiki yako’’ au ‘rafiki yao’’ majina yao” badala ya kuwaelezea kama “wavulana ” na “wasichana”, anasema Martinson.

Lakini mwanasaikolojia Vahrmeyer anasema kulingana na uzoefu wake wa kufanya kazi na wateja unaonyesha kuwa sio watoto wote waliolelewa katika malezi haya wanaotimiza malengo ya malezi , “Kwa watoto wanaohisi salama kutumia fursa waliyopewa na wazazi waosafari inaweza kuwa ile ya uvumbuzi.

Hatahivyo, kwa baadhi ya watoto, ukosefu wa utambulisho wa jinsia yao halisi unaweza kuleta, makangiko na wasiwasi,” anasema.

Changamoto zinazojitokeza zaidi

Kutokana na mazungumzo kuhusu maadili na ufanisi wa malezi ya kutozingatia jinsia, wataalamu wanakubali kuwa changamoto kwa wale walioamua malezi hay ani kukubali kujifunza jinsi watu wengine wanavyochukulia malezi hayo

 Martinson anasema mama yake amekuwa akiendelea mara kwa mara kuhoji mtindo wake wa malezi , akiuelezea kama wa “mgeni” au “wa ajabu” kwamaba waroro wake wamevuka mipaka ya kanuni za mavazi, na ansema anahangaika kuelewa kwamba Martinson hawezi kuzungumzia kuhusu jinsia ya utambulisho wa watoto wake hadi wao wenyewe wafanye hivyo

Ni jambo linaloendelea kusambaa?

Iwapo malezi ya wazazi ya kutozingatia jinsia yatakuja kukubalika na kuwa ya kawaida ni suala la mjadala unaoendelea miongoni mwa wafuasi na waangalizi wa malezi hayo.

Siever anadai kuwa mifano ya hivi karibuni ya malezi ya kutozingatia jinsia katika habari na mitandao ya kijamii huenda inachangia “ongezeko dogo la kukubalika ”. kwa malezi haya. Hatahivyo, kwa maoni yake,malezi ya aina hii hayatakubalika na jamii kwa ujumla hivi karibuni.

Hatahivyo, wengine , kama Martinson, wana matumaini zaidi kuhusu makadirio, hususan katika nchi kama vile Sweden, ambayo ina historia ya kuongoza katika kampeni za usawa wa jinsia na haki za wapenzi wa jinsia moja LGBTQ.

Katika miaka tangu alipompata mtoto wake wa kwanza, Martinson anasema ni wazazi wachache zaidi ambao husimama katika uwanja wa michezo wa wanapocheza watoto wake na kuulizia kuhusu jinsia za watoto wake.