Wanasayansi wanaeleza jinsi Dunia itakuwa na "Mwezi" wa pili kwa muda mfupi

Muda wa kusoma: Dakika 3

Wanasayansi wanasema dunia iko katika hali ya mshangao msimu huu: itapata mwezi mwingine.

Asteroidi (mwamba mdogo unaozungunga kwenye uzio wa jua) ndogo inatarajiwa kuingia kwenye uwanja wa sumaku ya Dunia, kwa muda kuwa "mwezi wa mdogo."

Mgeni huyu wa anga za juu atasalia katika mzunguko wa Dunia kuanzia Septemba 29, kwa miezi michache kabla ya kutoka kwa kwenye sumaku ya dunia tena tena.

Kwa bahati mbaya, mwezi wa pili (asteroidi) utakuwa mdogo sana na dhaifu kuonekana kwa jicho, na utahitaji darubini ya kitaalamu kuuona.

Asteroidi, ambayo wanasayansi wanaiita 2024 PT5, inatoka kwenye ukanda wa asteroidi ya Arjuna, ambayo ina miamba inayozunguka obiti sawa na ya Dunia.

Wakati mwingine, baadhi ya asteroidi hizi huja karibu na Dunia, na kufikia umbali wa maili milioni 2.8 (kilomita milioni 4.5) kutoka kwenye sayari yetu.

Wakati asteroidi kama hii ikisonga kwa kasi ndogo ya karibu kilomita 2,200 kwa saa, sumaku ya Dunia huweza kuinasa kwa muda katika mzunguko wa sayari yetu, watafiti wanasema. Na hicho ndicho hasa kilichotokea. Kuanzia wiki hii, asteroidi hii ndogo itazunguka Dunia kwa miezi miwili.

Dkt Jennifer Millard ameiambia BBC kuwa asteroidi hiyo itaingia katika mzunguko wa dunia Septemba 29, na inatarajiwa kuondoka tarehe 25 Novemba.

"Asteroidi haitafanya mzunguko kamili kuizunguka Dunia, bali itabadilisha mzunguko wake kidogo, na kisha kuendelea na njia yake," Millard alisema.

Asteroidi ni kama futi 32 (mita 10) za upenyo, ikiwa ni ndogo ikilinganishwa na mwezi wa Dunia, ambao ni takriban maili 2,100 (kilomita 3,474) za kipenyo.

Unaweza pia kusoma:

Kwa sababu ya ukubwa wake mdogo na muundo wa miamba iliyovunjika, watu duniani hawataweza kuiona isipokuwa wale watakaotumia vifaa vya binocular au darubini za nyumbani.

Darubini ya kitaalamu "itaweza kuiona, na kuna picha nyingi nzuri mtandaoni za mwezi huu mdogo ukisonga haraka sana katikati nyota," Millard anaongeza.

Mwezi mdogo umeonekana kabla, lakini wengi hawakuweza kufanikiwa kuutambuliwa.

Kuna miezi ambayo imetembelea mzunguko wa Dunia zaidi ya mara moja, kama asteroidi "2022 NX1" ilizunguka katika obiti ya Dunia mnamo 1981, na kurudi tena mnamo 2022.

Ikiwa utakosa fursa hii, huwenda usibahatike kuiona tena kwa karibu miaka thelathini. wanasayansi wanatarajia "2024 PT5" itarudi kwenye mzunguko wa Dunia tena mnamo 2055.

Millard anaelezea kwamba jambo hili "linaangaza wingi wa mfumo wetu wa jua na kiwango cha vitu ambavyo bado havijagunduliwa," kwa kuzingatia kuwa asteroidi ya kwanza kutembelea iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Alibainisha kuwa kuna "mamia ya maelfu ya vitu ambavyo bado hatujavigundua, kwa hivyo nadhani hii inaonyesha umuhimu wa uwezo wetu wa kufuatilia anga kila wakati na kugundua siri zaidi."[za angani]

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi