Jimbo la Marekani linalowavutia raia wa kigeni kwa pato kubwa

Chanzo cha picha, Jorge Luis Perez Valery
Suala la uhamiaji haramu linajadiliwa katika uchaguzi wa Marekani. Wagombea wa urais wa Marekani Kamala Harris na Donald Trump, wanasema kuwa watapunguza idadi ya wahamiaji haramu kutoka Mexico kuingia nchini mwao.
Hata hivyo, serikali ya Republican katika jimbo la Marekani inajaribu kuwavutia wahamiaji zaidi. Jimbo hili ni Alaska.
Mji mdogo wa uvuvi karibu na Copper River Delta katika Ghuba ya Alaska, chakula cha Mexico kinachoitwa 'Tacos Tortillas' hupatikana katika milo ya watu wanaoishi hapa.
Wahamiaji kutoka maeneo ya mbali huja hapa kufanya kazi katika viwanda vya usindikaji wa samaki vya Alaska. Watu wanaokuja hapa wanaweza kupata zaidi ya kile wanachopata katika katika nchi yao.
Edgar Vega Garcia, ambaye alikuja hapa kutoka Mexico, alisema kuwa alifanya kazi hapa kwa miezi 4 na kupata zaidi ya dola za Marekani 27,000 .
Kwa mujibu wa shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD), wastani wa mapato ya kaya nchini Mexico ni chini ya dola 16,269 (karibu rupia laki 13 ) kwa mwaka.
Mji wa Córdoba hupata joto la digrii ndogo kwa mwaka mzima. Mvua kubwa au theluji hunyesha kwa mwaka mzima.
Hakuna jua hapa kwa miezi miwili ya mwaka. Wenyeji wanaita kipindi hiki kama Polar Night (Wakati ambapo jua halichomozi).
Wakati wa majira ya joto, wenyeji hupata afueni kwani huondokana na baridi. Mwanzoni mwa majira ya joto, watu wa eneo hilo huvua samoni na aina nyingine za samaki.
Ushindani ni mkubwa sana kwa wakati huu ambapo watu hujitahidi kupata samaki wengi iwezekanavyo wakati wa siku chache za majira ya joto. Zaidi ya nusu ya ajira katika mji huu zinahusiana na sekta ya uvuvi.
Kampuni zinahitaji wafanyakazi zaidi wa kusindika, kufunga, na kuuza samaki. Kwa kuwa hakuna wafanyakazi wa kutosha wanaopatikana ndani ya nchi, wanaletwa hapa kutoka maeneo mengine.

Chanzo cha picha, ge Luis Perez Valer
Mishahara ya kuvutia kwa wataalamu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa mujibu wa wizara ya kazi, asilimia 80 ya wafanyakazi wa uvuvi wa Alaska ni wa kigeni. Wafanyakazi wanakuja hapa kutoka nchi nyingine za Marekani na nchi za kigeni.
Wengi wa wafanyakazi wa kigeni ni kutoka Ukraine, Peru, Uturuki, Ufilipino na Mexico.
Mishahara na utamaduni wa kazi ni sababu kuu zinazovutia wageni. Wageni wanasema kuwa mshahara ni mkubwa hapa kuliko katika nchi zao.
Mvuvi hupata dola 18 kwa saa. Unapofanya kazi kwa muda wa ziada unaweza kupata karibu $ 27 kwa saa. (Kulingana na Sheria ya kazi ya Alaska mfanyakazi hulipwa malipo ya ziada ya 50% ya mshahara)
Kampuni nyingi hapa hutoa malazi na chakula mara tatu kwa siku kwa wafanyikazi wao. Kwahivyo hawahitaji kutumia pesa nyingi huko Cordova.
Kampuni hutoa fursa kwa wafanyakazi kuweka pesa zao zilizopatikana.
Hakuna ukumbi wa sinema au duka la ununuzi huko Cordova. Ikiwa hali ya hewa sio nzuri kwa uvuvi, wavuvi hunywa na kucheza michezo ya kujiburudisha kwenye baa.
Cordova inaweza kufikiwa tu kwa usafiri wa meli au ndege. Kwahivyo kampuni zinazoajiri wafanaikazi huwalipia pesa za tiketi ya kwenda huko na kurudi nyumbani.
Hata hivyo, wengine wanasema maisha ya wafanyakazi katika viwanda vya samaki vya Cordova sio mazuri sana.
Watu wanne wanaishi katika chumba kilichotengenezwa kutoka kwa makontena ya meli za usafirishaji.
Kazi ni ngumu sana. Wafanyakazi hubadilishana zamu za kazi. Hufanya kazi kwa saa 18 au zaidi kwa kila zamu.
Wafanyakazi wanapaswa kupata maelfu ya kilo za samaki kwa siku.

Chanzo cha picha, Jorge Luis Perez Valery
Biashara kubwa ya samaki
Usindikaji wa samaki ni biashara kubwa huko Alaska. Viwanda vya uvuvi na dagaa vya serikali huchakata zaidi ya tani 2,000 za samaki kila mwaka, kulingana na Chuo Kikuu cha Alaska Fairbanks. Hii ni zaidi ya nusu ya sekta ya samaki ya Marekani.
Mahitaji ya wafanyakazi wa kigeni kufanya kazi katika sekta ya uvuvi ya Alaska ni kubwa. Serikali ya Marekani imeidhinisha ongezeko la visa za muda zilizotolewa kwa wafanyakazi wahamiaji wanaohitajika kufanya kazi hapa mwaka 2023.
Idadi ya visa zilizotolewa kwa wafanyakazi wahamiaji mwaka 2022 ni elfu 66. Lakini katika mwaka 2023-2024 idadi hii imeongezeka hadi laki 1 laki 30.
Edgar amekuwa akifanya kazi mwaka huu katika kiwanda kidogo cha kusindika samaki kiitwacho 'Kaskazini 60 Seafoods' huko Cordova. Mmiliki wa kampuni hii ni Rich Wheeler. Rich Wheeler alisema kuwa baadhi ya wafanyakazi wahamiaji wanaofanya kazi huko Cordova walikuwa na matatizo kwa sababu baadhi yao walikuwa wakitumia madawa ya kulevya na kupigana kati yao.
Alisema biashara yake imepanuka sana kutokana na wafanyakazi wahamiaji kutoka Mexico. Anasema biashara yake isingeweza kukua sana bila ya Mexico, ambao kila wakati hujitokeza kwa wakati.
Changamoto kubwa kwa wafanyakazi wengi wahamiaji ni kuacha familia zao na kufanya kazi masaa mengi huko Alaska. Rosa Vega, mama wa Edgar, amekuwa akija na kwenda Alaska kila mwaka kwa miaka 18.

Chanzo cha picha, Gorge Luis Perez Valery
Kama hakuna wahamiaji
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amesema wageni wanaiba ajira za Marekani. Kamala Harris alisema kwamba tutaongeza usalama mipakani na kuleta mabadiliko katika sera ya uhamiaji ili kudhibiti uhamiaji haramu.
Cordova ina idadi ya watu chini ya 3,000. Lakini idadi hii huongezeka mara tatu wakati wa majira ya joto.
Meya wa Cordova David Ellison anaamini kuwa wahamiaji sio tisho kwa ajira, lakini ni ufunguo wa ukuaji wa uchumi.
Alifanya kazi katika kiwanda hicho kwa miaka mingi.
Ellison alisema kuwa bila wahamiaji, samaki wanaovuliwa na watu wa eneo hilo wataoza na kuwa bure.
"Bila wahamiaji, hakutakuwa na mtu wa kusindika samaki. " Kama hakuna wavuvi, mji huu utakuwa ukiwa," alisema.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












