Tetesi za soka Ulaya Alhamsi: Arsenal yavutiwa na kiungo wa Aston Villa Morgan Rodgers

.

Chanzo cha picha, Getty Inages

Maelezo ya picha, Morgan Rodgers
Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal wanatathmini ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 23, lakini Aston Villa wanasema watamuuza Rodgers kwa ofa ya pauni milioni 80 pekee. (Sun),

RB Leipzig wamekubali makubaliano ya kibinafsi na kiungo wa kati wa Liverpool na England walio chini ya umri wa miaka 21 Harvey Elliott, 22, huku kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 22, akikaribia kukamilisha uhamisho wa kwenda Chelsea. (Florian Plettenberg)

Marseille wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Ugiriki Kostas Tsimikas, 29, ambaye anatarajiwa kuondoka Liverpool msimu huu wa joto. (Footmercato - In French}

Mshambulizi wa Manchester United na Denmark Rasmus Hojlund, 22, na kambi yake wameweka wazi kwa Napoli na RB Leipzig kuwa anapendelea kuhama kwa mkopo na makubaliano ya kumnunua. (Fabrizio Romano)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ramsu Hojlund

Nottingham Forest iko kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kulia wa Sevilla Mhispania Jose Angel Carmona mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sports)

Forest pia inachunguza uwezekano wa kuungana tena na mlinzi wa Poland mwenye umri wa miaka 28 na Aston Villa Matty Cash. (Athletic - Subscription Required)

Everton bado wanataka kuwasajili wachezaji wapya kabla ya tarehe ya mwisho - hasa winga - na wanaweza kutuma ofa nyingine kwa mshambuliaji wa Southampton Muingereza Tyler Dibling, 19. (Sky Sports).

Alex Moreno wa Aston Villa, 32, yuko mbioni kujiunga na Girona baada ya beki huyo wa kushoto wa Uhispania kukubali kupunguza mshahara wake. (Athletic - Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alex Moreno

Tottenham wanaongeza juhudi zao za kumnunua mlinzi wa Brentford na Ireland Nathan Collins, 24, ambaye pia amewavutia Liverpool. (Offside)

Bournemouth wameanza mazungumzo na Chelsea kuhusu mkataba wa mkopo kwa beki wa kati wa Ufaransa Axel Disasi, 27. (Sacha Tavolieri via Football Insider),.

BlueCo, kundi linalomiliki Chelsea na Strasbourg, limefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Paraguay Julio Enciso, 21, kutoka Brighton. (Athletic - Subscription Required)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla