Afghanistan: Wanaume walioanguka kutoka kwa ndege ya kijeshi ya Marekani

Familia ya Afghanstani yasimulia kuhusu mtoto wao wa kiume aliyeanguka kutoka katika ndege ya kijeshi ya Marekani.

Mwaka jana, matukio ya machafuko katika uwanja wa ndege wa Kabul yalitikisa dunia huku Waafghanistan, waliokuwa na hamu ya kutoroka utawala wa Taliban, walisukumana na kung'ang'ania upande wa ndege za kijeshi za Marekani.

Ndege ilipoanza kuruka, watu kadhaa waliuawa baada ya kuanguka kutoka angani.

Mwandishi wa BBC alienda kuona familia moja huko Kabul ambao wanadai haki kwa kifo cha mtoto wao wa kiume, ambacho wanasema kingweza kuzuilika kwa urahisi.