Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii (31.08.2022)

Arsenal bado inamtaka kiungo wa Leicester Youri Tielemans lakini hawajapeleka ofa hata moja kwa ajili ya kumnasa mchezaji huyo (Skysport)

Kiungo wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles yeye anakaribia kutua Southampton kwa mkopo wa mwaka mmoja (Romano).

Mazungumzo ya kina kuhusu uhamisho wa Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Barcelona kwenda Chelsea yameendelea leo, licha ya kwamba amepata majeraha yatakayomuweka nje kwa wiki kadhaa baada ya kuvamiwa na vibaka nyumbani kwake (@TheAthleticUK

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag: “Aaron wan Bissaka atasalia Old Trafford”. Anasakwa na vilabu vya Crystal Palace na Westham (Presser)

Wesley Fofana amejiunga rasmi na Chelsea kutoka Leicester kwa ada inayofikia £75m. (Skysport)