Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 11.07.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joao Neves

Paris St-Germain iko tayari kushindana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 19 Joao Neves. (Le10Sport – In French).

Barcelona wamekubali makubaliano kimsingi kwa mshambuliaji wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 21. (Sport – In Spanish}

Manchester United wana nia ya kukamilisha usajili wa beki wa Bayern Munich Mholanzi Matthijs de Ligt, 24, haraka iwezekanavyo baada ya Euro 2024. (Bild - in German)

Arsenal wamekubali ofa ya mkopo kutoka kwa Lazio kwa beki wao wa pembeni wa Ureno Nuno Tavares, 24 na kulazimika kumuuza kati ya £6m na £7m. (Mirror}

.

Chanzo cha picha, DAVIDPRICE

Maelezo ya picha, Nuno Taveres

Chelsea hawana nia ya kuanzisha kipengele cha kumnunua mshambuliaji wa Uhispania Dani Olmo mwenye umri wa miaka 26 katika klabu ya RB Leipzig kwa pauni milioni 50. (Sky Sports)

Beki wa kati wa Uingereza Jacob Greaves, 23, amekamilisha vipimo vya afya ili kuhamia Ipswich Town kabla ya kuondoka kutoka Hull City. (Sky Sports),

Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid huenda ndiko anakoelekea kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Juventus kumalizika mwezi uliopita. (Calciomercato – in Italy), nje

Marseille wanavutiwa na mshambuliaji wa Arsenal na Uingereza Eddie Nketiah, 25. (Footmercato – In French)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Xavi Simons

Bayern Munich wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons, 21, kutoka Paris St-Germain. (Sky Sports)

Monaco imekataa dau la euro 30m (£25.5m) kutoka kwa Nottingham Forest kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ufaransa Youssouf Fofana, 25, ambaye amekubali makubaliano na AC Milan. (Fabrizio Romano}

Kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 29, atakamilisha uhamisho wake kutoka Fulham hadi Bayern Munich katika muda wa saa 24 zijazo. (Sky Germany)

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla